wafanyakazi wenzake marehemu Nicodemus luther wakiwa wanalia kwa uchungu wakati wakiweka mashada
Shangazi wa marehemu akiwa analia kwa uchungu kanisani
Watu wawili akiwemo afisa Ugavi daraja la pili wa bunge wamezikwa jana katika makaburi ya Njiro mkoani hapa.
Watu hao amb ao ni Nivodemas Lather ambaye ni mfanyakazi wa bunge pamoja na Andrew Mkoalo walifarikia dunia juzi mara baada ya kupiga risasi na ndugu yao wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Katika maziko hayo ambayo yaliongozwa na Naibu Spika job Ndugai sanjari na baadhi ya wabunge na wafanyakazi wa bunge yalikuwa yametawaliwa na simanzi nzito huku kila aliehuthuria msiba huu akilaani kitendo hicho ambachi marehemu hawa wamefanyiwa.
Akiongea katika msiba huo mkurugenzi wa kamati ya ugavi bungeni Methew Kilapilo alisema kuwa wamepokea msiba huo kwa majonzi makubwa kwani ni kitu ambacho hakijawahi kutokea katika bunge.
Alisema kuwa marehemu enzi za uhai wake alikuwa mpenda watu amani pamojja na mchapakazi ivyo wamepoteza nguvu katika bunge na kitengo chake.
Aidha alibainisha kuwa kabla ya kifo chake marehemu aliwaaga baadhi ya wafanyakazi na kuwaambiwa anakwenda katika kikao cha familia ndipo walipopewa taarifa baadaye amefariki dunia mara baada ya kupigwa risasi.
Kwa upande wake mbunge wa Mbozi mashariki Godfrey Weston Zambi ambaye naye alihuthuria mazishi ya wanandugu hawa alisema kuwa wao kama wabunge haswa yeye binafsi amesikitishwa sana na tukio hilo na kuliita ni lakinyama kupita kiasi.
Alisema kuwa wamepokea msiba huu kwa masikitiko makubwa sana na umemgusa kila mbunge ambaye alikuwa anamjua marehemu na asiye mjua kwani marehemu alikuwa ni mtu wa upendo na watu.
"kwakweli napenda kuwasihi watanzania majirani ndugu pamoja na wengine wote kuwaombea sana ndugu zetu mungu azilaze mahali pema peponi na wafike sala huko waendapo"alisema Zambi
Aliongeza kuwa anapenda kuwasihi watanzania kuombea familia hizi ambazo zimeachwa gafla kwa wakati mmoja pasipo kutegemea.
Nae mombolezai aliyejulikakana kwa jina la Neema Rafaeli alisma kuwa kitendo hicho ni cha kinyama ambacho kwa binadamu yoyote asinge takiwa kumfanyia mwenzake kitendo kama hicho .
"iliyobaki tuwaombee kwa mungu tusilaumu sana kwani ni mipango ya mungu ndo maana ikawa "alisema neema.
Marehemu Nivodemas Lather ameacha watoto wanne pamoja na mjane huku marehemu Andrew Mkoalo akiwa ameacha mtoto mmoja na mjane.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia