Wananchi wa kata ya magugu iliyopo wilayani Babati mkoani Manyara wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kutoa maoni yao ya
mchakato wa kutafuta katiba mpya ya Tanzania,ambayo itawawezesha kuondoa kero
mbalimbali zinazowakabili.
Hayo
yalibainishwa na mbunge wa jimbo la Babati vijijini ,Vrajilal Jitu Son
wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Magugu kuhusiana na sakata
sima la katiba mpya.
Aliwataka
wananchi hao kujitokeza kwa wingi kushirikim katika sakata ili la
kupata katiba mpya kwani itawasaidia wao wenyewe kupanga sheria zitakazo
wasaidia.
Alisema wananchi wanatakiwa kuchangia maoni ya katiba mpya
ili kuweza kujua zaidi na kuisoma kwa makini kwani itawasaidi katika maisha yao
na kujua haki zao za msingi.
Alisema kuwa ni jukumu la kila
mwananchi kujitokeza katika kuchangia katiba hiyo pale ambapo atahitajika
kuchangia hivyo wasiogope kujitokeza kwani wanahaki na uhuru wa kutoa kero zao
za kimaendeleo ambazo zinawakabili.
Aliwataka wananchi hao kuacha
tabia ya kuropoka ropoka kwa kitu ambacho hawakifahamu pamoja na ushabiki
usiokuwa wa maana badala yake waifahamu kwanza katiba iliyopo kwani ndiyo
iliyowafikisha hapo sasa.
Pia katika sekta ya elimu aliwataka
wakazihao kujitahidi wapate shule ya sekondari ya kidato cha tano hivyo
wajitahidi angalau wapate kujenga shule mbili za kidato cha tano pamoja na
kuboresha shule za awali hadi sekondari ili wazazi wasipate gharama za
kuwasafirisha watoto wao katika mikoa mingineo.
Alisikitishwa na mkoa wa
Manyara kwa kuongoza kwa kufutiwa matokeo ya darasa la saba na kuiomba serikali
kuwafikiria ili kuweza kurudia mitihani hiyo pia wazazi wawaulize watoto wao
mbinu walizotumia kujaza mitihani hiyo.
Aliwataka wazazi pamoja an
walezi kufuatilia maendeleo ya watoto wao shuleni nasi kuwaachia walimu pia
wazazi wanatakiwa kufahamiana na walimu na walimu wanatakiwa kuwajua wazazi.
"Jamani tunatakiwa
tuhakikishe watoto wetu wanasoma na kufaulu kwani urithi wa milele kwa mtoto ni
elimu pekee na siyo kumrithisha mali,fedha, majumba, magari, mifugo kinachotakiwa
ni elimu itakayomsaidia katika maisha yake ya baadaye, ili aweze kujiajiri na kuondoka na
umaskini,’’ alisema Jitu.
Alisisitiza kwa kusema kuwa maadili yamepungua kwa vijana kutokana na kuiga mambo ya ulaya watu wanavaa
nguo za ajabu zinazoonyesha maumbile ya miili yao na kuwaacha nje,kwa wanaume
kushusha suruali huku nguo zao za ndani zikionekana,kulewa hovyo na kutoa
matusi makali.
Aidha alisema kuwa chanzo cha
mmomonyoko wa maadili nikutokana na wazazi kutowalea watoto wao katika misingi
ya kidini hivyo wanatakiwa kuwafundisha watoto wao maadili mema ya dini
zao pamoja na tamaduni ili kuweza kupata viongozi wazuri na waadilifu katika
ngazi ya jamii,kata,Taifa,wilaya na hata mikoa yao kwa ujumla.