Msanii mwenye umri
mdogo katika mziki wa kizazi kimpya Abuduli Change(dogo Janja) anayetamba na
kibao cha wanajua kama dogo janja anajua ameingia katika vita kubwa na wasanii wa mziki huo katika mkoa wa
Arusha Nigga wa Jambo Squad .
Wasanii hao wa hapa
mjini Arusha wanatoka katika mitaa maarufu ya Ngarenaro,Sombetini,kaloleni
pamoja na soweto wameamua kwa pamoja kumtangazia ubaya msanii huyo chipukizi.
Mmoja wa wasanii hao
kutoka katika kundi la Jambo Squad (Nigga ) alisema kuwa chanzo cha ubaya huo
ni kitendo cha msanii huyo kuwasaliti wasanii wa mziki wa kufoka foka hadi
kufikia hatua ya kujitangaza kuwa ametoka mkoa wa Kilimanjaro wakati yeye ni
Mrangi na amezaliwa katika mtaa wa Ngarenaro mkoani hapa.
Alisema kuwa mbali na
kuwakana wasanii wenzake wa mkoani hapa msanii huyo pia amediriki kuwatolea
lugha chafu kwa kupitia simu za mkoani na katika baadhi ya mitandao ikiwemo
Faccebook pamoja na BBM pamoja na kuwatishia baadhi yawasanii hao kwa kuwatumia
mabansa ili wawapige.
Aidha alikuwa yeye
mwenyewe kama Nigga anaweza kusema kuwa yeye ndo alimfanya msanii huyo aweze
kutoka hadi hapo alipofikia kwani kunavibao vingi ambavyo yeye mwenyewe
amemtungia dogo Janja.
"mimi naweza
sema hivyo kwakuwa dogo janja mimi nilikuwa namfanya kama mdogo wangu na kuna
vibao vingi ikiwemo kile cha sijafikia nimemtungia mimi lakini nashangaa sasa
ivi dogo ameenda bongo anatusahau kibaya
zaidi anatutukana na kusema kuwa ajatokea Arusha eti anajitangaza kuwa ametokea
Kilimanjaro kitu sio cha kweli"alisema Nigga.
Alibainisha
kinachosikitisha zaidi zaidi msanii huo anabaidilisha adi staili ambayo ndo
imemtoa kitu ambacho kinampotezea washabiki kwani dogo janja alikuwa anaimba
mziki wa kufoka foka akijitambulisha kama mtu wa Arusha lakini kwa sasa ivi
amebadilisha na anaimba muziki ambao ni wa kuiga na auendani naye.
"unajua dogo
atapotea kitu kimoja ameenda dar akajibadilisha kama mtu wa dar wakati alikuwa
anaimba muziki wa kiarusha adi kuongea mimi nilivyomtungia iyo muziki na kumpa
sikutaka anipe chochote ila nilimpa ili awakilishe ngarenaro na Arusha kwa
ujumla lakini ameenda uko Madee amembadilisha na kufanya aimbe kibongo bongo
,afu kibaya zaidi amemwambia asema ametokea kilimanjaro eti akamuita mangi
maiki mangi maiki nawakati ametokea urangini kibaya zaidi ameandika kwenye BBM
kuwa albamu yangu nunua ila ubeti wa kwanza ondoa kwakuwa ametunga Nigga ila mingine yote
nimeimba mimi afu mimi msinifananishe kama jambo squid maana jambo wanaimba
mashairi ya kuchekesha"alisema Nigga.
Alibainisha kuwa dogo
janja awezi kumfanya chochote na ata kwenye muziki amfiki kwani yeye anatunga
mwenyewe na kufundisha na siyo anatungiwa na kubainisha kuwa dogo janja
akumbuke muziki wa kwanza alioutoa wa sijafikia kufanya mapenzi ninani kampa na
katunga ndo aongee.
"nasema kuwa
mimi sitishiwi kwa chochote palipo na ukweli nasema ila napenda mwambia dogo
aendelee kunitumia watu walionifata leo ao mabaunsa na akae akijua kuwa yeye
anakipaji cha kutunga na kufundisha na anawatoto hadi wa vidudu awajui kusoma
lakini kawafundisha kuimba ivyo haimsumbui na madee na pia napenda kumwambia
madee asione vyaelea vimeundwa"alisema Nigga.
Gazeti lilizungumza
na msanii huyo Abuduli Change(digo Janja) kwa njia ya simu naye alisema kuwa
yeye ajasaliti Arusha na bado anaipenda Arusha na kamwe awezi kusaliti mkoa
aliotoka nakubainisha kuwa katika wimbo wake aliyosemaa anatokea Kilimanjaro ajakosea
kwani yeye anawakilisha kanda ya kaskazini
“nasema hivi mimi sijasaliti arusha na
ngarenaro ,na siwezi fanya ugomvi na mtu
maana siwezi jua nani atamsaidia mbele na katika swala la kumtumia mtu mimi
sijamtuia mtumwapige kiukweli sister yangu
na kwa upande wa kwenye BBM ni uongo sijaponda wasanii wa Arusha”alisema
Dogo janja.