BREAKING NEWS

Thursday, January 19, 2012

TPC YATOA BONASI


MENEJIMENTI ya kiwanda cha sukari cha TPC imetoa kiasi cha shilingi
bilioni 1.2 kwa wafanyakazi wake wa kudumu kama bonasi  itokanayo na
faida katika msimu wa kilimo 2010/2011  ili kuongeza tija katika
uzalishaji.

Katika taarifa iliyotolewa na ofisa mtendaji mkuu wa kiwanda hicho
Robert Baisac ilisema kuwa kutokana na faida hiyo kila mfanyakazi
amepata kiasi cha shilingi 693,000 kabla ya kukatwa kodi.

“Sidhani kama kuna kampuni nyingi Tanzania ambazo wanahisa wake
wanapenda kutoa kiasi hicho cha fedha kwenye faida yao kugawana na
wafanyakazi lakini kwetu hili tumekuwa tukilifanya kila mwaka”alsema
Baisaac.

Alisema falsafa ya wanahisa wa kiwanda hicho ni rahisi kwamba kiwanda
kikifanya vizuri kila mfanyakazi atazawadiwa na kwamba wafanyakazi wa
ngazi ya Sinior na wale wa ngazi ya juu nao pia wamepata bonasi yao
itokanayo na faida kulingana na makubaliano yao.

“Huu ni utaratibu tuliojiwekea endapo kampuni itafanya vizuri katika
uzalishaji kila mfanyakazi atapata zawadi kulingana na faida
iliyopatikana ,kumbuka kuwa iwapo kampuni itafanya vibaya,wote
tutapata kidogo,wanahisa na wafanyakazi pia”alisema Baisaac.

Alisema leo hii kampuni inafurahia hali hiyo kutokana na mambo mawili
ambayo ni uzalishaji mkubwa wa sukari na amani pia mahusiano mazuri
kazini yaliyopo hivi sasa.

Baisaac alisema mwaka 2010 kampuni iliweza kuweka rekodi ya mwaka kwa
kuzalisha sukari ya ziada kwa tani 86,000 kwa msimu kiasi ambacho
hakijawahi kufikiwa siku za nyuma toka kampuni hiyo ianze kuzalisha
sukari.

Alisema hata hivyo kampuni haikutarajia kurudia kupata mafanikio hayo
kutokana na uhaba wa mvua za kutosha hali iliyosababisha ukame kati ya
mwezi Oktoba na Novemba 2010 na pia mwezi machi na Aprili 2011.

“Kwa mshangao msimu huu uzalishaji ni mzuri kama sio mzuri sana zaidi
ya msimu uliopita,tunashurkuru jinsi tulivyozingatia kuoboresha
utendaji wetu katika maeneo yote kuanzia shambani ,usafirishaji
,kwandani,utwala na fedha”alisema Baisaac.

Aidha Baisaac alisema jambo la pili lililochangia kupatikana kwa faida
hiyo ni maelewano mazuri miongoni mwa menejimenti na wafanyakazi
pamoja na vyama vya wafanyakazi vya TASIWU na TPAWU.

“Tunashukuru jitihada tunazofanya kuweka uswa miongoni mwetu na uwazi
katika mawasiliano ,hali ya kuaminiana na mawasiliano mazuri yamezidi
kuimarika siku hadi siku.”aliongeza Baisaac.

Aidha Baisaac alisema kampuni ya TPC haitaishia hapo pia itaendelea
kuboresha kila eneo ,kiuchumi na kijamii si kwa ajili ya wanahisa
miongoni mwao ikiwa ni pamoja na serikali bali pia kwa jimii
inayozunguka kiwanda hicho.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates