MMBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI AFARIKI DUNIA

Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh. Jeremiah Sumari amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na maradhi ya uvimbe kichwani.Kuzaliwa Marehemu Jeremiah Sumari alizaliwa Machi 2 mwaka 1943 katika kijiji cha Akeri wilayani Arumeru Mkoani 
Arusha. 
Elimu yakeAlisoma elimu ya msingi kati ya mwaka 1950-1957 katika shule ya msingi Meru Magharibi mkoani humo mwaka 1958- 1964 alisoma katika shule ya sekondari ya Old Moshi Mkoani Kilimanjaro na baadae aliendelea na elimu ya juu huko Uingereza na kupata kama ifuatavyo- ACCA, CIS, Certificatein Marketing. Uk, Lincesed Broker (LR), CPA (Tanzania).Utumishi wake Mwaka 1996-2004 alikuwa Mkurugenzi wa bodi ya soko la Hisa Stokck Exchange mwaka 1998-2003 Trustee Privatization Trust, mwaka 1999-2006 alikuwa Mkurugenzi wa bodi Benki ya maeneleo ya Afrika Mashariki, mwaka 2005 mpaka sasa mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Januari 4 mwaka 2006 aliteuliwa kuwa Waziri wa kazi Ajira na Maendeleo ya vijana na mwaka 2008 mpaka 2010 alikuwa Naibu waziri wa Fedha na Uchumi.Marehemu Jeremiah Sumari alikuwa mbunge wa Arumaru Mashariki mpaka umauti ulipomkuta 
marehmu anatarajiwa kuzikwa January 23 mwaka huu uko mkoani Arusha 
Mungu ailaze roho yake mahali pema Peponi Amen

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post