BARAZA la Ardhi
na Nyumba mkoa wa Arusha, limeamuru wafanyabiashara 9 maarufu wenye
asili ya kiasia jijini hapa na kampuni ya chai
Tanzania(TTB), kuondolewa katika nyumba waliokuwa wamepanga.
Nyumba hiyo Ploti namba 2,Block M, inamilikiwa na kampuni ya Crown Holdings ya jijini Dar es alam na wametakiwa kulipa malimbikizo ya madeni na gharama za kesi hiyo baada ya kushindwa kulipa pango la nyumba hiyo kwa kipindi kirefu.
Hukumu hiyo imetolewa Desemba 15 mwaka 2011 na mwenyekiti wa baraza la Ardhi na nyumba , Michael Makombe, katika kesi namba 174 iliyofunguliwa na kampuni hiyo Agosti 13 mwaka 2007 ,ikiwalamikia waliokuwa wapangaji wake ambao ni wafanyabiashara wenye asili ya Kiasia, ikiwemo kampuni ya Chai nchiniTTB ,kwa kushindwa kulipa deni la pango kwa muda mrefu.
Akitoa
hukumu hiyo, Mwenyekiti huyo amesema kuwa ,baraza limeridhika na
ushahidi uliotolewa na upande wa utetezi kwamba walalamikiwa wameshindwa
kulipa deni la pango,hivyo wanapaswa kuondoka katika nyumba hiyo na
kulipa gharama zote za uendeshaji wa kesi hiyo na madeni wanayodaiwa.
Baraza
hilo limeiamuru kampuni ya wakala wa mahakama iitwayo Marcs
Investiment Limited ya jijini Arusha, kuwaondoa wapangaji hao ambao ni
10 waliokuwa wamepanga sehemu tofauti tofauti katika nyumba hiyo
iliyopo barabata ya uhuru.
Katika
hukumu hiyo Baraza limesema kuwa wadaiwa walishindwa kuthibitisha
katika madai yao ya msingi ya kuhusu kusudio la ongezeko la kodi ya
pango walikuwa wameweka pingamizi la kutoongezewa kodi mpya .
Wapangaji
hao wanadaiwa malimbikizo ya kati ya shilingi 150,000, hadi 260,000
ambayo ni kodi ya kila mwezi kulingana na ukubwa wa chumba kodi ambayo walikuwa wakiilalamikia na hivyo hawakulipa tangia walipofungua kesi hiyo.
Katika
kesi hiyo wapangaji hao walikuwa wakitetewa na makampuni mbalimbali ya
uwakili ikiwemo kampuni maarufu ya ,J.J. Mwale, ya jijini Arusha ambayo
hata hivyo ilikuja kujitoa na baadae ikaja kampuni ya Imboru Chembers
ya jijini Arusha, iliyowasilishwa na wakili Merinyo.
Wapangaji
walioondolewa kwenye nyumba hiyo ni Al-Hakim Shakir ambaye alikuwa
akimiliki duka kubwa la dawa za binadamu,K.A.Mohamedali, Muktaben
G.Daya, Nitesh V Nakeshri, Shah Lakamshi Meda, Nazm Karimbhaa, Asheri m
Ndambule ,Singh Noma,Vansantlala Dharamshi na kampuni ya chai, Tanzania
Tea Blenders TTB.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa kampuni ya kukusanya madeni ya Marcas
Investiments, Richard Nkanyemka alisema kuwa wao wametimiza kazi
waliopewa na mteja wao mara baada ya mahakama kutoa order ya wapangaji
hao kuondolewa katika nyumba hiyo.
Hata
hivyo Nkanyemka aliwataka wafanyabiashara hao kufuata taratibu za
kuchukua mali zao zilizoondolewa kwenye maduka yao baada ya shughuli ya
uvunjwaji wa maduka hayo kufanyika desemba 16,mwaka huu saa10
jioni,ambazo amezihifadhi kwenye ghala maalumu zikiwa salama.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia