AFISA MAENDELEO JAMII MANISPAA YA ARUSHA AFARIKI DUNIA



AFISA Maendeleo ya jamiii wa Manispaa ya Arusha David Ndauka amefariki dunia juzi jioni kwa Ugonjwa wa shinikizo la damu (heart attack) wakati akikimbizwa hospitalini  kwa matibabu, ambapo alikuwa akiuguwa ugonjwa huo kwa mda mrefu 

Akidhibitisha kutokea kwa msiba huo jana,Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha Estomih Chang'a amesema kuwa msiba huo ni wakusikitisha kwani marehemu alifariki  dunia ghafla jioni juzi  wakati akikimbizwa hospitalini kwa Dr.Urassa

"Ni kweli bw.ndauka amefariki jana(juzi)jioni kwa shinikizo la damu ni ugonjwa aliokuwa nao kwa muda na kwa bahati mbaya alifariki dunia wakati akikimbizwa hospitalini"alisema Chang'a kwa uchungu huku akisikitika

Chang"a aliongeza kuwa wamempoteza mtu muhimu sana kwani yeye alikuwa ni mtaalam aliyeisaidia Halmashauri hiyo kuunganisha vijana katika makundi na kuwasaidia kupata usajaili wa vikundi ambavyo kwa sasa Halmashauri inavitumia vikundi hivyo kwa shughuli mbalimbali ili kuweza kupunguza wimbi la ajira kwa vijana

Aliongeza kuwa marehemu kabla ya kukutwa na mauti alikuwa ni mwanafunzi wa chuo cha Mt.Meru university akisomea masters na taratibu za mazishi zinaendelea kwa kushirikiana na ndugu wa marehemu huko nyumbani kwake Kambi ya chupa

"Nimapema sana kusema wanazika lini ila msiba huo upo nyumbani kwake Kambi ya chupa na taratibu za mazishi zinaendelea tutawaarifu"alisema Chang'a

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post