MWENYEKITI wa Chama cha mpira wa
miguu mkoani Manyara (MARFA) Charles Mngodo amevitaka vyama vya michezo vya
wilaya za mkoa huo kufanya uchaguzi wao mapema ili kuwa na viongozi
wanaotambulika kisheria.
Akizungumza na waandishi wa
habari mjini Babati,Mngodo alivipongeza vyama vya michezo vya wilaya za
Simanjiro na Hanang’ kwa kufanya chaguzi zao na kupata viongozi wapya hivi
karibuni.
Mngodo alisema kuwa vyama vya
wilaya vya mkoa huo ambavyo hadi hivi sasa havijafanya uchaguzi wake ni
Babati,Mbulu na Kiteto ambao wanatarajia kufanya uchaguzi wao hivi karibuni.
“Chama cha wilaya ya Kiteto
(KIDFA) hakina matatizo kwani kinatarajia kufanya uchaguzi wake Januari 15
mwaka huu hii ni changamoto kwa vyama vingine ambavyo bado havijachagua
viongozi wake,” alisema Mngodo.
Alisema chama cha mpira wa miguu
wilayani Babati (BADFA) kinakabiliwa na changamoto kubwa ya viongozi wake kuwa
na migogoro kila mara isiyo na tija hivyo wajipange kikamilifu kwa ajili ya
kufanya uchaguzi na kumaliza migogoro.
Alisema migogoro kwenye michezo
inasababisha kurudisha nyuma michezo kutokana na kushindwa kupanga mikakati ya
maendeleo na kubaki kusuluhisha migogoro na malumbano yasiyo na maana wala
faida.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia