WAFANYAKAZI WA TPC WAJIFUA KWA AJILI YA MBIO ZA KILIMANJARO MARATHONI


wageni walioshiriki mbio za Kilimanjaro marathoni za mwaka jana 


WAFANYAKAZI wa kiwanda cha sukari  TPC cha wilayani Moshi wameanza
maandalizi kwa ajili ya mbio za kimataifa za Kilimanjaro Marathoni
ambazo zinataraji kufanyika mwishoni mwaka  Februari 26 mwaka huu.

Ofisa Mafunzo na ustawi wa kiwanda hicho Peter Magera alisema katika
taarifa yake kuwa maandalizi hayo ambayo ni pamoja na mazoezi yana
lengo la kupata wakimbiaji watakaokiwakilisha kiwanda katika mbio
hizo.

Alisema mazoezi hayo ambayo yameanza katika uwanja wa michezo wa
Limpopo ulioko kiwandani humo yatakuwa chini ya mwalimu wa mchezo wa
riadaha hususani mbio ndefu ambaye hata hivyo hakuweka wazi jina lake.

“Tunafanya mazungumzo na mwalimu wa mbio ndefu  aliyebobea katika fani
hiyo na mazoezi yataanza kesho(leo)katika uwanja wetu , hivyo nitumie
nafasi hii kuwaalika wale wote watakaopenda kushiriki kujitokeza
katika mazoezi hayo”alisema Magera.

Alisema baada ya mazoezi ya wiki mbili timu itakayo kiwakilisha
kiwanda itachaguliwa ambapo kila mchezaji atalipiwa gharama zote
ikiwamo kiingilio ,usafiri na pia kupatiwa vifaa vya mazoezi na
mashindano.

“Wale watakao chaguliwa kwenye timu ya kampuni watalipiwa gharama zote
kuanziia mazoezini hadi wakati wa mashindano kwa hiyo nafasi hii ni
vyema wafanyakazi wakaitumia vizuri ili kuhakikisha kampuni mwaka huu
inafanya vizuri katika mbio hizo”alisema Magera.

Magera alisema kwa wale wataopenda kushiriki katika mazoezi ya mbio
hizo watatakiwa kufika katika ofisi ya Mafunzo na ustawi wa jamii kwa
ajili ya kujiandikisha ili kupata idadi ya watu wataoanza mazoezi ya
pamoja.

"Mwaka huu tunataria kufanya vyema katika mbio hizi ,sina shaka
tutaotoa mshindi wa mbio ndefu kutokana na maandalizi tuliyoaanza
mapema na hakika pia mwalimu tuliyempata atatufikisha katika ushindi
wa mwaka huu"alisema Magera.

Mbio za Kilimanjaro Marathoni ambazo mwaka huu zinaadhimisha miaka 10
tangu zianzshwe zimekua miongoni mwa matukio makubwa zaidi ya
kimichezo katika eneo la Afrika Mashariki na Kati huku zikiwa ni
kichocheo cha utalii kwa nchini na kwa wakazi wa mikoa ya Kilimanjaro
na Arusha.

Wadhamini wa mbio hizo ni kampuni ya bia Tanzania (TBL)kupitia bia
yake ya Kilimanjaro Premium Lager, GAPCO Tanzania na Vodacom Tanzania
huku wadhamini wengine wakiwa ni  CFAO Motors, Tanga Cement,
TanzaniteOne, Keys Hotel, Precision Air, Kilimanjaro Water, TPC Sugar,
Southern Sun Hotel, KK Security na Bodi ya Taifa ya Utalii.

Mbio za Kilimanjaro huandaliwa na Kampuni ya Wild Frontiers ya Afrika
Kusini na kuratibiwa na Kampuni ya Executive Solutions wakati Chama
cha Riadha cha Taifa na kile cha Kilimanjaro husadia kuratibu na kutoa
msaada wa kiufundi.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post