BREAKING NEWS

Tuesday, January 31, 2012

OLDIVAI YATWAA UBIGWA MASHINDANO YA KUHAMASISHA UPIMAJI UKIMWI


mchezaji wa timu ya Oldivai akiwa anapokea zawadi marabaada ya kutangazwa mshindi kwenye mashindano ya kuhamasisha ukimwi

Timu ya Oldivai ya jijini hapa imeweza kuibuka kidedea mara baada ya kuifunga timu ya Kaloleni magoli 2-1  katika mashindano ya uhamasishaji kupima ukimwi yaliyoandaliwa na Taasisi ya YES ya jijini hapa kwa kushirikiana na chama cha mpira wa miguu wilaya ya Arusha (ADFA).
 
Mashindano hayo ambayo yalifanyika kwa muda wasiku moja kwa kuzikutanisha timu 10 za jijini hapa yalifanyika katika uwanja wa sheikh Amri Abeid  na timu hii ya Oldavai iliweza kunyakuwa kombe mara baada ya kuibuka na ushindi.
 
Akiongelea mashindano hayo mratibu wa michezo hiyo Samweli Mpenzu alisema kuwa  nia haswa ya kuandaa mashindano hayo ni kuhamasisha wananchi kupima ugonjwa wa Ukimwi .
 
Alisema kuwa waliamua kuhamasisha  kwa njia hii ya michezokwani watu wengi wamekuwa wakipenda michezo haswa mpira wa miguu hivyo waliamini swala hili litapokelewa kwa kasi kubwa kwani watu wangi ambao wanaingia katika michezo wataenda kupima na kujua afya zao.
 
Alisema kuwa wao kama Tasisi ya Yes kwa kushirikiana na chama cha mpira wa miguu wilaya ya Arusha (ADFA) wataendelea kuandaa mashindano kama haya ili kuweza kuwahamasisha watu kwenda kupima na kujua afya zao.
 
“unajua ugonjwa huu umekuwa ukienea kwa kasi  na watu wengi ambao wamekuwa wakiugua ni vijana hivyo tumeamua kuanza kuwapima vijana na kuwahamasisha wapime ili kuweza kujua afya zao na pia tunatoa mafunzo ya jinsi ya kuepuka na maambukizi haya ya ugonjwa wa kukimwi”alisema Mpenzu.
 
Alitaja baadhi ya timu ambazo zilipokea swala hili kwa mwitikio mkubwa na wachezaji wake wengi kujitokeza kupima afya zao kabla ya kuingia uwanjani kucheza kuwa ni pamoja na Inter Stax, Roling stone ,Cidt,Young life ,kaloleni, inter sports, olduvai kids pamojana Arusha talenti.
 
Akiongea na gazeti hili mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Arusha (ADFA) Charles Mwaimu alisema kuwa  mashindano haya yatawasaidi vijana  ambao ndio wamekuwa wakiongoza kupata maaambukizi haya ya virusi vya ukimwi kwani watakuwa wenapata mafunzo ya kujifunza jinsi ya kujikinga na maambukizi hayo.
 
Alisema kuwa wao kama chama cha mpira wa miguu wilaya ya Arusha watashirikiana kwa dhati na taasisi hii ya Yes ilikuweza ku endelea kuandaa mashindano kama haya ambayo wanaimani yatawasaidia vijana kwa ujumla
 
Katika mashindano hayo timu ya Oldvai ili weza kuibuka kidedea cha magoli 2-1 mara baada ya kuifunga kalolini  na timu ya inter sport iliweza kushika nafasi ya tatu.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates