mchezaji wa timu ya Oldivai akiwa anapokea zawadi marabaada ya kutangazwa mshindi kwenye mashindano ya kuhamasisha ukimwi
Timu ya Oldivai ya jijini hapa imeweza kuibuka kidedea mara baada ya kuifunga timu ya Kaloleni magoli 2-1 katika
mashindano ya uhamasishaji kupima ukimwi yaliyoandaliwa na Taasisi ya
YES ya jijini hapa kwa kushirikiana na chama cha mpira wa miguu wilaya
ya Arusha (ADFA).
Mashindano
hayo ambayo yalifanyika kwa muda wasiku moja kwa kuzikutanisha timu 10
za jijini hapa yalifanyika katika uwanja wa sheikh Amri Abeid na timu hii ya Oldavai iliweza kunyakuwa kombe mara baada ya kuibuka na ushindi.
Akiongelea mashindano hayo mratibu wa michezo hiyo Samweli Mpenzu alisema kuwa nia haswa ya kuandaa mashindano hayo ni kuhamasisha wananchi kupima ugonjwa wa Ukimwi .
Alisema kuwa waliamua kuhamasisha kwa
njia hii ya michezokwani watu wengi wamekuwa wakipenda michezo haswa
mpira wa miguu hivyo waliamini swala hili litapokelewa kwa kasi kubwa
kwani watu wangi ambao wanaingia katika michezo wataenda kupima na kujua
afya zao.
Alisema
kuwa wao kama Tasisi ya Yes kwa kushirikiana na chama cha mpira wa
miguu wilaya ya Arusha (ADFA) wataendelea kuandaa mashindano kama haya
ili kuweza kuwahamasisha watu kwenda kupima na kujua afya zao.
“unajua ugonjwa huu umekuwa ukienea kwa kasi na
watu wengi ambao wamekuwa wakiugua ni vijana hivyo tumeamua kuanza
kuwapima vijana na kuwahamasisha wapime ili kuweza kujua afya zao na pia
tunatoa mafunzo ya jinsi ya kuepuka na maambukizi haya ya ugonjwa wa
kukimwi”alisema Mpenzu.
Alitaja
baadhi ya timu ambazo zilipokea swala hili kwa mwitikio mkubwa na
wachezaji wake wengi kujitokeza kupima afya zao kabla ya kuingia
uwanjani kucheza kuwa ni pamoja na Inter Stax, Roling stone ,Cidt,Young
life ,kaloleni, inter sports, olduvai kids pamojana Arusha talenti.
Akiongea na gazeti hili mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Arusha (ADFA) Charles Mwaimu alisema kuwa mashindano haya yatawasaidi vijana ambao
ndio wamekuwa wakiongoza kupata maaambukizi haya ya virusi vya ukimwi
kwani watakuwa wenapata mafunzo ya kujifunza jinsi ya kujikinga na
maambukizi hayo.
Alisema
kuwa wao kama chama cha mpira wa miguu wilaya ya Arusha watashirikiana
kwa dhati na taasisi hii ya Yes ilikuweza ku endelea kuandaa mashindano
kama haya ambayo wanaimani yatawasaidia vijana kwa ujumla
Katika mashindano hayo timu ya Oldvai ili weza kuibuka kidedea cha magoli 2-1 mara baada ya kuifunga kalolini na timu ya inter sport iliweza kushika nafasi ya tatu.