TAN COMMUNICATION MEDIA WANAMPANGO WA KUSHIKA NAFASI YA KWANZA TANZANIA KATIKA SWALA ZIMA LA KURUSHA MATANGAZO

 wafanyakazi wa  Tan Communication Media wakiwa katika kikao chao cha kujadili jinsi ya kuboresha vipindi vyao
 niliingia studio nikamukuta mkaka akiendelea kuwapa wasikilizaji raha
 libeneke lilitinga katika chumba cha kuandalia   vipindi na kukuta kila mfanyakazi akiwa anaandaa kipindi chake na wa habari alikuwa anajiandaa kujifua ili akasome habari
 muonekano wa jengo la Tan Communication Media kwa mbele
 walipokea mgeni kwa ukarimu mzuri
 walionyesha furaha kila mmja apo ni baadhi  ya watangazaji wakiwa  pamoja na mdada wa libeneke woinde
watangazaji wa Radio 5 wakiwa katika pozi

 Kampuni ya Tan Communication Media inayomiliki kituo cha radio 5 kilichopo mkoani  arusha  kimejipanga vyema katika kuhakikisha kuwa  mwaka 2012 kinakuwa kituo bora cha matangazo Tanzania nzima.

Akizungumzia mikakati hiyo mkuu wa vipindi katika kituo hicho Flora Mallya amesema moja ya mikakati waliyojiwekea ni pamoja na kubaoresha vipindi ili viwe bora sanjari na kufanya kazi kama timu ili kufikia malengo waliyojiwekea.

Bi,Mallya amesema kuwa ili radio hiyo kuwa bora zaidi pia kampuni hiyo ina mpango wa kuwapeleka watangazaji mafunzo ya mda mfupi ndani na nje ya nchi ili kuwawezesha kufanya vizuri zaidi katika vipindi vyao.

Aidha ameongeza kuwa ili mfanyakazi aweze kufanya kazi kwa bidii ni lazima kampuni ijali wafanyakazi wake ili nao pia wajisikie kuwa ni moja ya kati ya sehemu ya kampuni hiyo.

Kwa upande wao wafanyakazi wa kituo hicho kinachokuja kwa kasi katika tasnia ya utangazaji hapa nchini wamesema wamejipanga vyma kuhakikisha kuwa wanafanya mambo makubwa na mazito na kuifanya radio hiyo kuwa tishio hapa nchini
.
Radio 5 ni moja kati ya vituo vichache binafsi vyenye jingo la kisasa kabisa (Broadcasting Hause).

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post