Rais wa wanasheria Tanganganyika France Stola akiwa na Jaji mkuu wa Tanzania Othman Chande wakiwa wanaelekea sehemu maalumu waliokuwa wametengewa kwa ajili ya kuongea na waandishi wa habari
Raisi wa wanasheria wa Tanganyika France Stola akiwa anaongea na vyombo vya habari kuhusiana na mkutano unaoendelea katika ukumbi wa Simba ulioko katika jengo la mikutano la kimataifa AICC jijini Arusha
Jaji Mkuu wa Tanzania Othman
Chande akiwa anajibu maswali ambayo aliulizwa na waandishi wa habari
mawakili wa kike waliouthuria katika mkutano huo wakiwa wanabadilishana mawazo wakati wa mapumziko
Mahakama nchini zimetakiwa kutoahirisha kesi mara kwa mara ikiwa hakuna sababu za msingi za kufanya hivyo
kwa kuwa inachelewesha wahusika kupata haki zao kwa wakati.
Hali inatokana na mahakama nyngi hapa nchini kuahirisha kesi
mara kwa mara bila sababu za msingi hali ambayo haileti tija kwa wenye kudai
haki.
Hayo yamesemwa na
Jaji Mkuu wa Tanzania Othman
Chande wakati akifungua mkutano mkuu wa kwanza wamwaka wa chama cha wanasheria Tanzania bara uliofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa kimataifa(AICC) mkoani Arusha.
Jaji chande amesema kuwa kesi zinaweza kuahirishwa ikiwa
kuna sababu za msingi kama msiba au wakili
ambaye yupo katika kesi hiyo ana kesi nyingine lakini sababu nyingine ambazo si
za msingi zisisababishe kesi kuahirishwa ili kesi hizo zimalizike kwa wakati.
Pia Jaji chande amesema kuwa kuna changamoto nyingi ikiwa ni
pamoja na wananchi wenye uwezo wa kawaida kupata haki yao ya msingi ya wakili
pindi wanapokuwa wanakabiliwa na kesi kubwa kama ubakaji ambazo adhabu zake ni kubwa kama vile kifungo cha maisha ambapo walitakiwa kupata mtetezi lakini
kutokana na mawakili wa serikali kuwa wachache wanakosa huduma hizo.
"napenda
pia kuwahasa hawa mawakili kuwa katika kazi yao wasiangalie jicho la
mteja tu bali waangalie na upande wapili kwani watu wote tunafanya kazi
kwa pamoja"alisema Chande
Kwa upande wake Rais
wa chama cha wanasheria Tanganyika Francis Stola alisema kuwa mkutano huo ni wa kutathimini utoaji
haki na majukumu ya mahakama ambapo ameiomba serikali upande wa mahakama kutenga fungu la fedha za
kutosha ili mahakimu na majaji waweze kufanya kazi zao kwa umakini zaidi.
Hata hivyo amesema
kutokana na kukosekana kwa fungu la fedha la kutosha hali hiyo inapelekea wanasheria
wengi kupokea rushwa na kupelekea haki kupotea kwa wananchi ambao waniotegemea
mahakama.
Aidha stola ameeleza kuwa kukosekana kwa vitendea kazi kama maktaba na kukosekana kwa vitabu vya sheria ni tatizo
pindi mahakama inapotaka kutoa maamuzi.
Alisema
kuwa katika mkutano huo pia watajadili baadhi ya changamoto ambazo
wanakutana nazo ikiwa ni pamoja na kujadili jinsi ya kuzuia rushwa
katika mahakama mbalimbali ,jinsi ya kukarabati majengo ya mahakama
pamoja na jinsi ya kuwasaidia wananchi wa kima cha chini jinsi ya
kutatua kesi zao.
Stola alisema mada ambazo zitakazotolewa kuwa ni pamoja na
mfumo wa uendeshaji wa kesi za madai,njia gani iweze kutumika ili bunge liweze
kutunga sheria ambazo zitakuwa bora,mfumo wa uwendeshaji wa kesi a jinai na
nyingine nyingi.
mkutano huo unatarajiwa kumalizika kesho ambapo wanasheria
kutoka Tanzania bara wameshiriki ili kuhakikisha kuwa wanakuwa na mchango wao
ili wananchi wenye uwezo wa chini wanapatiwa haki zao.
Aidha
Allitaka serekali kuwapa nafasi wananchi katika swala zima la katiba
mpya na watoe fursa kwa kila mwananchi kuchangia katiba hiyo.
"ili
katiba iwe katiba ni wajibu wa kila mwananchi kuchangia maoni yake hapo
ndio tutaiita katiba tofauti na hapo kwakweli sijui"alisema Stolla.