ZAIDI ya wakulima 60 wa vijiji vya Kisimiri,Olkung'wado na Miririni
vilivyopo kata ya leguruki na ngarenanyuki wilayani Arumeru wamenufaika na
mafunzo ya kilimo bora cha mbaazi na kupatiwa mbegu za mahindi lishe lengo
likiwa ni kuwawezesha kujikwamua kiuchumi na kujipatia lishe bora .
Mafunzo hayo yaliyoendeshwa na wataalamu kutoka chuo cha utafiti wa mbegu
selian na kufadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Africa Amini Alama
kutoka nchini Austria ambapo mkurugenzi wa shirika hilo bi Christine
Wallner alisema kuwa mafunzo hayo yatawafanya wakulima kuondokana na hali
ya utegemezi katika jamii sambamba na kuwafanya kupata lishe bora.
Bi Christine alisema kuwa kutokana na wakulima wa eneo hilo kuathirika kwa
ajili ya viwatilifu vilivyopo kwenye kilimo chao wanachotegemea cha nyanya
iliwabidi kubuni kilimo kingine ambacho hakitaweza kuwaathiri ambacho ni
cha mbaazi na mbegu za mahindi lishe bora ambapo ilimpasa kuwafadhili
wakulima hao kwa kuwapatia mafunzo bure na mbegu ili waweze kunufaika na
kilimo hicho.
Aliongeza kuwa kutokana na mafunzo ya mbegu za mahindi lishe walizopatiwa
wakulima hao yatawasaidia kupata vitamini kwa kuwa watu wengi wamekuwa na
mazoea ya kula vyakula visivyokuwa na vitamini hivyo kupitia mbegu hizi
zitaongeza vitamini hasa kwa watoto na familia kwa ujumla
"Wakulima hawa waliopatiwa mafunzo haya ya kilimo bora cha mbaazi na mbegu
za mahindi lishe yatawasaidia sana katika kujikwamua kiuchumi na
kuondokana na umaskini kwani kilimo hiki hakina madhara kama kilivyo
kilimo cha nyanya hivyo zingatieni elimu mliyoipata iliiweze kuwasaidia
."alisema Christine
Nae mjumbe wa shirika hilo bw Jafferson Severua alisema kuwa wameweka
mkakati wa kuwajengea wakulima hao ghala la kuhifadhia mbaazi hizo mara
wavunapo ili waweze kukusanya huko kwa lengo kusubiri kuuza kwa bei nzuri
kwa kuwa wakulima wengi wanakabiliwa na sehemu za kuhifadhia mazao yao mara
wavunapo hivyo kusababisha kuuza kwa bei ya hasara.
"wakulima hawa wakishavuna mazao yao watakusanya kwenye ghala ambalo
tunatarajia kulianza hivi karibuni na baadae watachukua kama walivyokusanya
ambapo kila mkulima atajua idadi ya kiasi chake alichokiweka ili wauze kwa
bei wanazozitaka wenyewe kuliko kuuza kwa hasara kwa ajili ya kukosa sehemu
ya kuihifadhia"alisema Severua

Habari hii imeandikwa na Rose Kitosio wa Libeneke la kaskazini
Nawaonea wivu wana vijiji hao wa Arumeru, waliopata hayo mafunzo natamani na mimi ningekuwepo, nipo huku Dar nikihitaji hao ndugu zetu waje huku kwetu watupatie hayo mafunzo, nifanyeje? tutajipanga na wananchi wenzangu mimi kwa sasa ni mkulima wa mboga mboga,naomba nisaidiwe utaratibu, asante kwa blog kutupatia mambo ya muhimu sana kwa ustawi wa maisha yetu. email:emmanueltwaha@yahoo.com
ReplyDelete