Makampuni 100 ya kilimo na nafaka kutoka nchi mbalimbali balani Afrika , yanatarajiwa
kushiriki maonyesho ya kilimo na biashara yanayotarajiwa kufanyika
jijini Arusha yatakazoshirikisha nchi kumi za Afrika ambazo ni
wanachama wa baraza la nafaka la kanda ya Afrika Mashariki(EAGC).
Aidha
maonyesho hayo yatalenga zaidi kutoa mafunzo kwa wakulima ,kuhusu
kilimo ,biashara na kuweza kuonyesha ni jinsi gani wakulima hao wataweza kunufaika zaidi na mazao yao na jinsi ya kuweza kupata masoko ya ndani na nje ya nchi.
Mkurugenzi Mkuu wa baraza hilo ,Gerald Masika aliyasema hayo katika uzinduzi wa maonyesho ya kilimo biashara yatakayofanyika jijini Arusha,
Masika
aliongeza kuwa maonyesho hayo yanaandaliwa na EAGC kwa kushirikiana
na kituo cha utafiti wa kilimo cha Selian (SARI)kilichopo Ngaramtoni
ya chini jijini Arusha na yatafanyika katika kituo hicho cha utafiti.
Alisema kuwa, maandalizi ya maonyesho
hayo yanatarajiwa kugharimu kiasi cha dola za kimarekani 80,000 hadi
90,000 ambapo mkulima amepewa kipaumbele zaidi kushiriki kikamilifu
kutokana na umuhimu wa biashara ya kilimo na mazao.
Alifafanu
kuwa, maonyesho hayo pia yatasaidia kupata utatuzi wa changamoto
inayowakabili wakulima ikiwa ni pamoja na kukabilina na mbegu feki
ambazo zimekuwa zikiingizwa kwenye mzunguko wa biashara za mbegu kwa
mawakala wa pembejeo.
Aidha
aliongeza kuwa wakulima nchini watajifunza njia mojawapo ya kukabiliana
na soko la am,zao kufutaia serikali kuzuia zoezi la uvushwaji wa mazao
mbalimbali hususani mahindi nje ya nchi kwani changamoto hiyo imewafanya
wakulima wakate tamaa ya kulima na wengine kushia kupata kupata hasara.
Naye Mkurugenzi wa EAGC nchini
, David Tuhoye aliwataka wakulima nchini kujitokeza kwa wingi katika
kushiriki maonyesho hayo ili waweze kukutana na wenzao wa kutoka nchi
mbalimbali na kubadilishana uzoefu.
Aidha
alisema kuwa, kwa sasa wakulima kwa hapa nchini wanakabiliwa na
changamoto kutokana na uuzawaji wa mahindi kutokana na serikali kupiga
marufuku uvushwaji wa mahindi nje ya nchi hali ambayo imesababisha
mahindi mengi kubakia kwenye maghala .
Alitolea
mfano katika mji wa Kibaigwa kwamba mahindi tani elfu 10 yapo kwenye
maghala ambapo wakulima wameshindwa kuyapatia soko la uhakika kutokana na serikali kuuzia uvushwaji wa mahindi nje ya nchi na hivyo kujikuta wakipata hasara kubwa sana .
‘’Kwa
kweli wakulima wengi wamekuwa wakilalamikia hali ya serikali kupiga
marufuku swala hilo kwani wengi wao wamebakia maskini kutokana na kuwa
wengi walikuwa wakitegemea bidhaa hiyo kutimiza malengo yao
mbalimbali,hivyo kupitia maonyesho hayo yatawezesha kuwasaidia
kuzungumzia changamoto hiyo pia ,hivyo ni jukumu la wakulima kujitokeza
kwa wingi’’.alisema Tuhoye.