Amiri na mbashiri mkuu wa jumuia ya waislamu wa Ah madiyya nchini,Tahir Mohmood Choudhly katikati, sheikh mkuu wa Ahmadia mkoa wa morogoro Bakari kaluta(kushoto) na sheikh mkuu kanda ya kaskazini Mzafara Ahamad(kulia)wakiwa kwenye picha ya pamoja siku ya kongamano la amani lililofanyika mjini hap,sanjari na uzinduzi wa msikiti wa mkoa wa ahmadiyya mwishoni mwa wiki
VIONGOZI
wa madhebebu mbalimbali ya dini ya kiislamu mkoani Arusha, wameongoza kongamamo
maalumu la kulaani mauaji yanayofanywa na kikundi kidogo cha kiislamu chenye
msimamo mkali cha Boko haramu nchini Nigeria dhidi ya madhebebu ya dini ya kikristo.
Wakizungumza
kwenye
kongamano la amani lililofanyika mwishoni mwa wiki katika msikiti Ah
madiyya jijini hapa,walidai kuwa nakuna maagizo ya mwenyezi mungu
yanayotoa
mamlaka kwa kikundi hicho ama mtu yoyote kutekeleza mauaji hayo dhidi ya
waumini wa dini nyingine.
Amiri na mbashiri
mkuu wa jumuiya ya waislamu wa Ahmadiyya nchini,Tahir Mohmood Choudhly
aliwaomba waislamu kote duniani kuungana na kulaani vitendo vya kinyama kama
hivyo vinavyofanyika kwa kutumia mgongo wa uislamu.
Aliwaomba
watanzania kuwalilia wananchi wote waliouawa kutokana na kikundi hicho
cha Boko haramu nchini Nigeria,na aliiomba serikali nchini humo,
kukakikisha inadhibiti mauaji hayo na kukishighulikia kikundi hicho
kinachotumia mgongo wa uislamu.
‘’sisi
waislamu tufike mahali tuelezane ukweli kwani matukio mengi ya uvunjifu wa
amani yakiwemo kujilipua yanasababishwa sana na waumini wenzetu ,hakuna
maandiko yanayoagiza dini ya kiislamu iteketeze dini nyingine ‘’alisema
Choudhly.
Aidha
aliongeza kwa kuwataka viongozi wa
madhehebu ya dini nchini kusimama imara katika kutetea amani na kujiepusha na
uchochezi,kwani taifa linawategemea sana katika kuepusha machafuko yanayoweza
kuibuka.
Katika hatua nyingine, aliwataka
wananchi kuheshimu viongozi waliopo madarakani na kuacha kupinga kila kitu
kinachotamkwa na kiongozi aliyeko madarakani, badala yake watoe mchango wa
kusukuma maendeleo ya taifa hadi utakapo fanyika uchanguzi mwingine.
Naye
Sheikh mkuu wa Ahamadiyya kanda ya kaskazini,Mzafara Ahamad,alisema kuwa lengo la
kongamano hilo lililowashirikisha viongozi mbalimbali wa madhehebu mbalimbali ya
dini ya kiislamu nchini ni kutoa mada ya kuomba amani na kulaami mauaji ya
kikatili yanayoongozwa na kikundi haramu cha kiislamu nchini Nigeria.
Alisema
kuwa kongamano hilo lilienda sanjari na uzinduzi wa msikiti huo wa Ahmadiyya
muslim Jamaint uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 70 kwa ajili ya ukarabati
ulioanza mwishoni mwa mwaka jana.
Kwa upande
wa sheikh mkuu wa Aha madiyya mkoa wa Morogoro,Bakari Kaluta,aliwataka viongozi wa dini
nchini kutawala kiuadilifu huku
wakiongozwa na mwenyezi mungu katika mahubiri yao na kuacha kuwa sehemu ya
kuleta mitafaruku ya kidini.
Ameyasihi
madhebebu ya dini kuwa na utaratibu wa kuandaa makongamano ya kuomba amani
,kwani bila hivyo nchi itaelekea kubaya kwakuwa baadhi ya viongozi wa dini
wamekuwa wakitumia vibaya maandiko matakatifu kwa kuhubiri uvunjifu wa amani
kwa maslahi yao binafsi.
Naye meya
wa jiji la Arusha ,Gaudence Lyimo aliyekuwa mgeni rasimi katika kongamano
hilo,aliyasifu madhehebu ya dini ya kiislamu kwa kuandaa kongamano hilo la kuomba amani ,aliwatia moyo viongozi hao
kuwa serikali inatambua mchango wao na inawaungamkono kwa jambo hilo.
Aliwasihi
viongozi hao wa dini kuwa sehemu ya serikali katika jitihada zake
za kuhakikisha kuwa amani inapatikana kwa kila mtu hapa nchini na duniani kote.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia