MLALAMIKAJI KATIKA KESIYA KUPINGA MATOKEO YA UBUNGE AELEZA KUWA DKT BATILDA BURIAN ALIKUWA NA MIMBA YA LOWASA

HATIMAYE  kesi dhidi ya Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini Bw Goodbless Jonathan  Lema inaendelea mjini hapa huku mlalamikaji wa pili akielezea mahakama kuwa wakati za kampeni Bw Lema alidai aliyekuwa mgombea mwenza kwa tiketi ya chama cha mapinduzi Dkt Batilda Burian alikuwa na mimba ya Waziri mkuu mstaafu Bw Edward Lowasa huku akiwataka wananchi wasimpe kura kwa kuwa jimbo litauzwa na Lowasa.
 
Hayo yalielezwa na Bi Agness Mollel mbele ya  Jaji mfawidhi kutoka Sumbawanga ambapo mlalamikaji huyo alieleza kuwa  Bw Lema aliyasema hayo wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2010 katika eneo la Big  Sister Mwanama
 
Bi Agness alieleza mahakama kuwa Lema aliyasema hayo wakati akiomba kura za Ubunge kwa jimbo la Arusha mjini ambapo hali hiyo ilimdhalilisha sana  dkt Batilda Burian.
 
Alieleza kuwa kutokana na hali hiyo ilimfanya yeye binafsi kuona kuwa Dkt Batilda amezalilishwa kijinsia , kidini, na kikabila  hata kama ni kipindi cha uchaguzi mkuu wa Raisi, Wabunge, na Madiwani.
 
“nakumbuka  Mbunge alisema hayo wakati akiomba kura lakini pale mwanama kwa big sister na kutokana na khali hiyo ya kusema kuwa alikuwa  na mimba ya Lowasa asipewe kura mimi ilinilazimu kufungua mashitaka kwa kuwa ni haki yangu ya msingi”alisema bi Agness ambaye ni mlalamikaji wa pili.
 
Kwa upande wa wakili wa mbunge wa jimbo la arusha mjini Bw Methody Kimomogoro alimtaka mlalamikaji huyo wa pili kuimbia mahakama juu ya sababu zake za kufungua kesi wakati Dkt batilda ambaye ni mlengwa kushindwa kufungua kesi.
 
Bw Kimomogoro alisema kuwa mlengwa halisi katika kesi hiyo ambaye ni Dkt Batilda ndiye aliyetakiwa kutoa malalamiko hayo dhidi ya Bw Lema tofauti na wanachama wa chama hicho  ambaye ndiye aliyeambiwa maneno hayo.
 
Bw Kimomogoro alibanisha kuwa mpaka sasa hakuna kielelezo chochote kile kinachoeleza kuwa Dkt Batilda amemlalamikia Bw Lema katika nyakati za kampeni tofauti na wanachama ambao walishitaki na kutaka matokeo yatenguliwe.
 
Hataivyo Wakili wa Serikali Bw Timon Vitalis alimuuliza mlalamikaji  huyo juu ya malalamiko yake dhidi ya mbunge wa jimbo la Arusha, hususani juu ya ushawishi wake juu ya kufungua kesi ambapo mlalamikaji huyo alikiri kufanya hivyo.
 
“hapa unaeleza mahakama jinsi ulivyoenda kwa Dkt mara baada ya uchaguzi kuisha na mlikuwa watu watatu ambao ndio ninyi walalamikaji kwa maana hiyo wewe ulimshawishi Dkt kufungua kesi lakini Dkt Batilda hakungua ila wewe na wenzako ndio mliofungua Kesi”alisema Bw Vitalisi.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post