Msemaji wa TFF Boniface Wambura
Timu
ya AFC ya Arusha imeshindwa kutokea kwenye mechi ya Kundi C ya Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) dhidi ya 94 KJ iliyokuwa ichezwe jana (Februari
15 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani.
Kwa
mujibu wa Kanuni ya 21 ya FDL timu yoyote inayoshindwa kufika kituoni
na kusababisha mchezo husika kutochezwa itashushwa daraja hadi Ligi ya
Taifa na matokeo ya michezo yake yote itafutwa ili kutoa uwiano sahihi
kwa timu zilizobaki kwenye mashindano.
Si
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), msimamizi wa ligi hiyo
Kituo cha Pwani wala Kamishna wa mechi hiyo Ramadhan Mahano waliokuwa na
taarifa yoyote ya mapema juu ya AFC kushindwa kufika kituoni.
AFC
ambayo mbali ya kushushwa daraja inatakiwa kulipa faini ya sh. milioni
moja kabla ya kucheza Ligi ya Taifa msimu ujao. Sh. 500,000 kati ya hizo
zitakwenda kwa timu ya 94 KJ iliyoingia gharama za kujiandaa kwa mechi
hiyo ambapo wapinzani wao hawakufika uwanjani.
Kundi
C la ligi hiyo sasa linabakiwa na timu nne baada ya Manyoni FC ya
Singida nayo kushuka daraja kwa kushindwa kucheza mechi yake dhidi ya
Polisi Tabora iliyokuwa ifanyike Februari 12 mwaka huu Uwanja wa Ali
Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Timu
zilizobaki katika kundi hilo ambalo baada ya mbili kujitoa hakuna
itakayoshuka daraja ni 94 KJ ya Dar es Salaam, Polisi Tabora, Polisi
Morogoro na Rhino FC ya Tabora.
libeneke lilizungumza na baadhi ya wapenzi wa soka wa mkoa wa Arusha nao walisema kuwa wamesikitishwa sana na kitendo cha timu hii kushuka daraja kwani kwani walikuwa wanaitegemea kama ndio timu ya wananchi.
"kwakweli tunasikitishwa sana kwa kitendo cha timu hiikushuka daraja kwani ndiho timu tulikuwa tunaitegemea katika soka la mkoa wa Arusha sasa watu wacheche wamesababisha hata timu yetu ikashuka tunalaani sana.
libeneke pia lilizungumza na mmoja wa waandishi wa habari Mahmoud Ahmad alisema kuwa amesikitishwa sana kuona timu ambayo ilikuwa ndio kioo cha michezo katika mkoa wa Arusha ikiachwa yatima hadi kufikia kushuka daraja.
alitoa ushauri kwa viongozi wa mkoa kuandaa timu mapema na kutafuta wafadhili kwani wameona mechi tatu za timu ya Jkt Oljoro zikipotea kitu ambacho sio jambo zuri na inaashirika kuporomoka kwa soka mkoani Arusha.
"viongozi wasipoangalia kwa umakini tutabaki kuwa wasindikizaji katika soka hapa nchini kitu ambacho ni aibu kubwa sana kwani awali katika mpira wa mkoa huu kulikuwa na soka la zuri ambalolilimsisi mua kila mmoja lakini kwa sasa limeondoka hamna soka kabisa tunaelekea kuwa watazamaji wa timu zingine tu " alisema Mahamoud
Aidha alitoa wito kwa viongozi ambao lawama kubwa zimetupiwa kwao kuwa wajirekebishwe na watafute kazi zakufanya na sio kutegemea mpira jambo ambalo linawafanya wakae kupigiana fitina katika soka na sio kusaidia soka la mkoa wa Arusha
Timu hii ya AFC imekuwa ni timu ya kung'ang'aniwa na watu ambao wengi wao wamekuwa wakiifanya timu hii shamba la bii hali iliyofanya kuifikisha timu hii hapa ilipo na katika timu hii wachezaji wenyewe wamefanya kazi ya ziada na kujituma vilivyo kwani kutokana na malumbano ya viongozi hao na wanachama yalipelekea hata wacheza kwenda kucheza mechi bila kula na wengine kuishi hata bila ya kupewa posho za kujikimu