WALEMAVU WAMUOMBA RAIS KUWEKWA KATIKA MCHAKATO WA KUSAKA KATIBA MPYA

Watoto ambao ni walemavu wa macho(vipofu ) wakiwa wanaelekea kupata kifungua kinywa hakipo pichani wakati wa mapumziko ya semina
Apa watoto ambao ni walemavu wa ngozi (Albino) wakiwa wanabadilisha mawazo 
Mwalimu wa watoto ambao ni hawasikii(viziwi) akiwa anaendelea kuwatafisiria watoto hao wakati mada ikiendelea
 
 
Jamii ya watu wenye ulemavu wameomuomba Raisi wajamuhuri ya muungano waTanzania Jakaya Mrisho Kikwete kuteuwa wawakilishi wawtu wenye ulemavu ili kuingiakatika mchakato wa kutoa maoni ya undwaji wa katiba mpya.
 
 mkurugenzi wa shirikala walemavu linaloshuhulikia haki za kisheria za maendeleo ya jamii na uchumi Gidion Mandesi wakati wa semina ya siku moja ya watoto wanoishi na ulemavu.
 
Alisema kuwa wanamuomba raisi kutumia busara katika kuunda tumehiyo ya watu 32 kuwa najapo watu watatu ambao ni walemavu ambao watawawakilisha wenzao katika mchakato huo.
 
Alisemakuwa kunawalemavu wengi ambao wana elimu ya kutosha na wanauwezo wa kutoa maoni yao kwa niaba ya wenzao hivyo wangefurahi sana kama nao wangeshirikishwa katika sakata hilo la kutafuta katiba mpya.
 
'ili katiba iwe ya haki kwa kila mwananchi ni lazima kila mtu apewe nafasi ya kuchangia maoni yake kwa hiyo tunaomba sana raisi atushirikishe na sisi walemavu katika mchakato huu wakusaka katiba ili nasisi tuweze kuibariki katiba hiyo "alisema Mandesi
 
Aidha alibainisha kuwa iwapo Raisi atateuwa wawakilishi wenye ulemavu kuingia katikatume hiyo basi ushirki wo utakuwa ni bora nawataweza kutoamaoni mazuri ili katiba hiiyo itoe fursa pia kwa watanzania wenye ulemavu.
 
Mandesi aliwataka watanzania wenye ulemavu kujiandaa kutoa maoni yao ili katiba hiyo iweze kuwasaidia na kuwanufaisha watanzania na kizazi cha kesho.
 
Hatahiyo alitoawito kwa watanzania wote kuwapatia fursa kwa kuwa wanaulemavu wanauwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko katika nchi ya Tanzania .

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post