WATAKIWA KUPIGANIA CHAMA KISHINDE


katibu wa UVCCM  wilayani Monduli  Ezekiel Mollel wa kwanza kushoto akiwa anafafanua jambo Mwenyekiti wa UVCCM wilayani Monduli Julias Lazer wapi katika mkutano wa vijana wilayani humo


Wananchi wa jimbo la Arumeru mashariki wametakiwa kudumisha amani na utulivu  haswa katika kipindi hichi cha uchaguzi .

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa UVCCM wilayani Monduli Julias Lazer wakati akiongea na vijana wa chama hicho katika mkutano wa  vijana wa kuandaa mikakati ya uchaguzi wa  UVCCM  kuanzia ngazi ya kata hadi taifa uliofanyika  wilayani humo.

Alisema kuwa wakifanya hivyo wataweza kupata fursa yakuchagu kiongozi bora mwenye ridhaa ya wananchi na sio anaetokana na ubabe na vitisho ambavyo vitaambatana na umwagaji damu.

Alisema kuwa iwapo watafanya hivyo watakuwa wamedumisha umoja kama wana Arumeru ambao ni wa msingi kuliko vyama.


Pia aliwataka Wanachama wa chama cha mapinduzi kumaliza  tofauti zao na kuunganisha  nguvu katika kutafutia ushindi chama chao na sio kuanza kulumbana katika kipindi hichi cha uchanguzi  wa jimbo la Arumeru Mashariki.

Alisema kuwa kipindi hichi sio cha kulumbana bali ni kipindi cha kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mbalimbali za chama pamoja na za jimbo la Arumeru  mashariki.

''unajua malumbano yakiendelea  haswa ya jimbo hili ambalo linauchaguzi  ndio tutawapa nafasi wapinzani wetu kutushinda kwa sababu pale tunapo gombana ndio ambapo tunawapa nafasi wao kupenya na kuzidi kukusanya wanachama wengi ngoja niulize kwani ni mwananchi gani atakubali kupigia kura chama ambacho wao wenyewe wana lumbana ivyo ni wajibu wa kila mmoja kuwa makini katika kipindi hichi"alisema Lazer

Alibainisha kuwa na ikiendelea hivi  kwa sababu siku ya siku bila uwanachama chama kita kuwa ni bure na akabainishwa kuwa iwapo watapoteza jimbo la Arumeru hawatakuwa na sababu ya kuitwa wananchama kwani kinachompa mtu kuitwa mwanachama ni kukipatia chama ushindi tu na sio vinginevyo hivyo ni wajibu wa kila mwanachama wa chama hivyokuhakikisha anajito vilivyo.

Kwa upande wake katibu wa UVCCM wilayani Monduli Ezekieli Mollel aliwata vijana wa chama hicho kujitokeza kwa wingi kuchukuwa fomu za kugombea nafasi mbalimbali za umoja wa vijana wa chama hicho kuanzia kata hadi taifa.

Alisema kwa kipindi hichi kila kijana anauwezo wa kugombea nafasi iwapo tu atakuwa ametimiza mashariti ya kuwa mgombea ivyo aliwataka vijana wote wajitokeze kwa wingi


1 Comments

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

  1. Big u Woinde! hii blog ninavyooona inazidi kuwa improved kila siku zinavyokwenda. keep it up and try to update us with latest news fro Kilimanjaro & Arusha!

    Bill Mwageni
    B.o. Box 4241,
    Dar es Salaam
    Tanzania.

    ReplyDelete
Previous Post Next Post