MASHAIDI WAENDELEA KUTOA USHAIDI KESI YA KUPINGA MATOKEO INAYOMKABILI MBUNGE WA ARUSHA MJINI


 Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akihutubia wananchi wake

Kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge jimbo la Arusha Mjini imesikilizwa leo katika Mahakama Kuu kanda ya Arusha ambapo mashaidi katika kesi hiyo walitoa ushaidi wao huku watu waliofika mahakamani hapo kuangua vicheko kutokana na ushaidi uliotolewa na mashaidi

Awali shaidi wa tisa katika kesi hiyo Bw.Iddy Hussein alisema mbele ya Jaji wa mahakama hiyo Gabriel Rwakibarila  kuwa baada ya kuwasili katika eneo la mkutano wa adhara eneo la Elerai, alikutana na maneno mazuri mwanzoni ambapo baadaye maneno mabaya(kashfa) yaliibuka jambo ambalo lilimfanya asiendelee kusikiliza sera ya chama cha chadema

"Sikumbuki kampeini ilifanyika lini na kumalizika lini nachojua mimi ni siku ya uzinduzi tu na sijawahi kuskia mikutano ya vyama vingine ikifanyika isipokuwa chadema"alisema shaidi namba tisa alipokuwa akihojiwa na wakili wa walalamikiwa Bw.Method Kimomogoro

Jaji alimtaka shaidi huyo kuelezea mahakama siku ya tuki hilo ni timu gani ilikuwa ikicheza ambapo shaidi huyo alisema  kuwa siku hiyo anakumbuka ilikuwa ni  mechi ya Manunited v Chelsea ambapo Chelsea walifungwa mabao 3 kwa bila,kutokana na majibu ya shaidi huyo watu waliokuwepo mahakamani hapo kuangua kicheko

Pia Shaidi wa kumi Bw.Salvatory Christopher, aliieleza  kuwa mdaiwa wa kwanza Godbless Lema hakumtaja aliyempa ujauzito aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM, Dk Batilda Burian, bali waliofanya hivyo ni wananchi waliohudhuria mkutano wake eneo la Ngusero, kata ya Sombetini, Manispaa ya Arusha

Akiongozwa na wakili wake, Modest Akida anayesaidiana na Alute Mughwai kuwawakilisha wadai katika shauri hilo, shahidi huyo alidai kumsiki Lema akisema Dk Burian hakustahili kupewa fursa ya kuwakilisha bungeni  jimbo muhimu kama Arusha kwa sababu alikuwa na ujauzito wa Mzee wa Moduli ambaye hakumtaja.


Shahidi huyo aliyedai kuwa mwanachama hai wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliieleza mahakama kuwa kauli hiyo ya Lema kuhusu mimba ya Dk Burian ilipokelewa kwa furaha na waliokuwa wakimsikiliza ambao walikuwa ni mchanganyiko wa watu wa rika na jinsi mbalimbali.

Awali wakili Kimomogoro alipokuwa akimhoji shahidi wa tisa alidai hoja juu ya ndoa na udini dhidi ya Dk Burian zilianzishwa na kuenezwa na wana CCM waliokuwa wakimuunga mkono, Felix Mrema aliyeangushwa kwenye kura za maoni ambao hawakufurahishwa na mtu wao kuangushwa katika mchakato wa kura za maoni ndani ya chama.

Bw.Kimomogoro allidai wafuasi wa Mrema ndio walioanza kumwandama Dk Burian kwa kuzusha na kueneza suala la yeye kuolewa na Mzanzibari na siyo kweli kwamba mteja wake Lema ndiye aliyeanzisha na kusambaza hoja hizo zinazolalamikiwa mahakamani na wapiga kura watatu waliofungua shauri hilo namba 13/2010 mahakamani.


Hoja ya wakili Kimomogoro aliyelazimika kutoa nakala ya gazeti la Mtanzania kuthibitisha madai yake ilikuja baada ya shahidi wa tisa Idd Husein kuieleza mahakama kuwa alimsikia  akiwataka wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni uliofanyika Septemba 6, mwaka juzi eneo la Elerai kutokubali kumchagua mtu aliyeletwa kugombea ubunge Arusha kwa mapenzi binafsi kwani baada ya uchaguzi angerejea Zanzibar alikoolewa na kuacha jimbo bila uwakilishi.

Katika shauri hilo Mwanasheria mkuu wa serikali ambaye ni mdaiwa wa pili katika shauri hilo anawakilishwa na mawakili Timon Vitalis na Juma Masanja.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post