VIONGOZI
wa dhebebu la Ah madiyya nchini wamewasihi waiislamu wenzao kote nchini
,kuungana na kuomba dua la amani kuiombea nchi ili kuepusha matukio
mbalimbali ya uvunjifu wa amani , ambayo yamekuwa yakienda kinyume na
maandiko matakatufu yaliyopo kwenye Quran .
Wakizungumza
kwenye kongamano la amani lililofanyika katika
msikiti Ah madiyya jijini hapa,walidai kuwa hakuna maagizo ya mwenyezi
mungu yanayotoa mamlaka kwa kikundi ama mtu yoyote kutekeleza mauaji
dhidi ya waumini wa dini nyingine.
Kiongozi
mkuu mwenye cheo cha Amiri na mbashiri mkuu wa jumuiya ya waislamu wa
Ahmadiyya nchini,Tahir Mohmood Choudhly aliwaomba waislamu kote duniani
kuungana na kulaani vitendo vya kinyama vinavyofanyika kote duniani
hususani nchi chenye uislamu kwa madai ya kutaka haki.
Aliwaomba
watanzania kuwalilia wananchi wote waliouawa kutokana na machafuko
mbalimbali yanayoendelea katika nchi za uislamu na kukilaani
kikundi kidogo wa wanamigambo cha Boko haramu nchini Nigeria,
kinachotekeleza mauaji kwa kisingizio cha kufuata maagizo ya uislamu
yalioko kweneye Quruan.
‘’sisi
waislamu tufike mahali tuelezane ukweli kwani matukio mengi ya uvunjifu
wa amani yakiwemo kujilipua yanasababishwa sana na waumini wenzetu
,hakuna maandiko yanayoagiza dini ya kiislamu iteketeze dini nyingine
‘’alisema Choudhly.
Aidha aliongeza kwa kuwataka viongozi
wa madhehebu ya dini nchini kusimama imara katika kutetea amani na
kujiepusha na uchochezi,kwani taifa linawategemea sana katika kuepusha
machafuko yanayoweza kuibuka.
Katika
hatua nyingine, aliwataka wananchi kuheshimu viongozi waliopo
madarakani na kuacha kupinga kila kitu kinachotamkwa na kiongozi aliyeko
madarakani, badala yake watoe mchango wa kusukuma maendeleo ya taifa
hadi utakapo fanyika uchanguzi mwingine.
Naye
Sheikh mkuu wa Ahamadiyya kanda ya kaskazini,Mzafara Ahamad,alisema
kuwa lengo la kongamano hilo lililowashirikisha viongozi mbalimbali wa
madhehebu mbalimbali ya dini ya kiislamu nchini ni kutoa mada ya kuomba
amani .
Alisema
kuwa kongamano hilo lilienda sanjari na uzinduzi wa msikiti huo wa
Ahmadiyya muslim Jamaint uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 70 kwa
ajili ya ukarabati ulioanza mwishoni mwa mwaka jana.
Kwa upande wa sheikh mkuu wa Aha madiyya mkoa wa Morogoro,Bakari Kaluta,aliwataka viongozi wa dini nchini kutawala kiuadilifu huku wakiongozwa na mwenyezi mungu katika mahubiri yao na kuacha kuwa sehemu ya kuleta mitafaruku ya kidini.
Ameyasihi
madhebebu ya dini kuwa na utaratibu wa kuandaa makongamano ya kuomba
amani ,kwani bila hivyo nchi itaelekea kubaya kwakuwa baadhi ya viongozi
wa dini wamekuwa wakitumia vibaya maandiko matakatifu kwa kuhubiri
uvunjifu wa amani kwa maslahi yao binafsi.
Naye
meya wa jiji la Arusha ,Gaudence Lyimo aliyekuwa mgeni rasimi katika
kongamano hilo,aliyasifu madhehebu ya dini ya kiislamu kwa kuandaa
kongamano hilo la kuomba amani ,aliwatia moyo viongozi hao kuwa serikali inatambua mchango wao na inawaungamkono kwa jambo hilo.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia