JKT OLJORO YALIZWA KATIKA UWANJAWA NYUMBANI

 Baadhi ya viongozi na wadau wa soka wa mkoa wa Arusha wakiwa wanaangalia mechi ya JKT Oljoro na Ruvu Shooting leo katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid
 Washabiki wa timu ya Jkt Oljoro wakiwa wanashangilia timu hao hii yote ni kuipa morali timu
 wachezaji wa timu ya JKT Ruvu wakiwa wanatoka uwanja kwenye mapumziko
 wachezaji wa timu ya JKT Oljoro wakiwa wanatoka uwanjani
 katika mechi hiyo kulikuwa na waandishi wa habari nao waliojitokeza kuangalia wa kwanza kuliani ni Ramathani Sywayombe akiwa na afisa habari wa mkuu wa mkoa anayemfata wakiwa wanafatilia mechi kwa makini
 Mashabiki nao walijitokeza kibao kuangalia timu yao
 wa kwanza kulia ni Katibu wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Arusha  Zakayo Mjema akifuatwa na mwaandishi wa habari mkongwa Mr.Mwala pamoja na muamuzi wakiwa wanabadilisha mawili matatu wakati mechi ikiendelea
 mchezaji wa Jkt Oljoro aliyevaa bluu akichuana na mchezaji wa Jkt Ruvu katika mechi hiyo
 hapa ni dokta wa timu ya JKt oljoro akiwa na wachezaji wamekaa katika benchi la timu
 mtanange balaa akuna aliyekuwa ankubali kushindwa
 waamuzi wakiwa wanatoka uwanjani mara baada ya mpira kuisha
 wachezaji wa timu ya Jkt Ruvu wakiwa wanashangilia ushindi wa bao moja kwa bila
 apo kigodeko wa kwanza akiwa ameketi anaangalia mpira kwa makini mara baada ya kutolewakupumzika


Timu ya JKT Oljoro ya jijini hapa ambayo imeshindwa leo kujitamba nyumbani mara baada yakufungwa katika uwanja wa nyumbani na timu ya JKT Ruvu  Goli 1-0  mechi ambayo ilichezwa katika uwanja wa kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid jijini hapa

Timu hiyo ambayo imefugwa mfululizo leo ikiwa mara ya tatu katika mechi yake ya leo  imeshindwa kujitamba mara baada ya kuonyesha kiwango  kidogo cha mpira hali iliyofanya kuwauzi washabiki wa soka wa timu hiyo.

mchezaji ambaye ameweza kuimaliza timu hiyo na kuifanya iongeze uchungu wa kufungwa ni mchezaji  Mohamed Banka ambaye aliweza kuinyuka timu hiyo goli hilo katika dakika ya 64 ya mchezo mara baada ya kuwazidi mbio mabeki wa timu ya Jkt oljoro.

Libeneke lilizungumza na kocha wa timu ya Jkt Oljoro  Chales Kilinda naye alisema kuwa amefurahi sana kushinda mechi hiyo kwani alikuwa anacheza ugenini.

Alisema kuwa katika mechi hiyo alikuwa anacheza kwa tahadhari kubwa kwani alikuwa analinda kutofungwa tena kama alifungwa katika mechi yake ya mwisho ambayo alicheza na Azam ambapo alisema kuwa katika mechi hii alijaza viungo wengi uwanjani ili  kuweza kuipatia timu yake ushindi.

Kocha huyu alilalamikia uwanja wa Sheikh Amri Abeid nakusema kuwa uwanja huu pia umechangia yeye kushindwa kupata magoli mengi kwani uwanja huu ni mbovu kupita kiasi 

Nilimtafuta kocha wa timu ya JKt oljoro ili azungumzie mechi hii lakini kwa bahati mbaya sikumpata kwani mara baada ya mechi kuisha hakuonekana amepita wapi

Nilibahatika kuzungumza na katibu wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Arusha Adam Broun naye alisema kuwa anashangazwa sana na ucheza ji wa timu hii wa siku ya leo kwani sio kawaida yake .

Alibanisha kwa kusema kuwa kufungwa ni matokeo ya kawaida kwaiyo hawana budi kuyapokea   ila alilaumu uwanja huo nakusema kuwa uwanja ndio chanzo kikubwa kilichochangia timu hii ikifungwa ivyo aliomba uongozi wa chama cha mapinduzi kurekebisha uwanja huo kwani ni mali yao.








Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post