" ninaimani na ccm oya oya oya "uwo ni wimbo ambao vijana walikuwa wanaimba kabla ya kutoa tamko
mwenyekiti wa Uvccm mkoa wa Arusha,James Ole Millya,mwenyekiti
wa Uvccm wilaya ya Arumeru akiwa anatoka kwenye mkutano huku akiimba nyimbo ya chama chake
walipotoka nje walianza kujadili katika vikundu mikakati ya kutetea jimbo lao
mwenyekiti wa Uvccm mkoa wa Arusha,James Ole Millya katikati ,mwenyekiti
wa Uvccm wilaya ya Arumeru,Esther Maleko wa kwanza kulia na kushoto ni Ombeni
Pallangyo ambaye ni mwenyekiti wa Uvccm kata ya King”ori wilayani Arumeru pamoja na jimbo la Arumeru mashariki
MGOGORO unaofukuta ndani ya jumuiya ya umoja wa
vijana wa CCM(Uvccm) wilayani Arumeru mkoani Arusha umeingia katika sura mpya
baada ya uongozi wa jumuiya hiyo kuitisha kikao cha dharula na kutoa tamko la kumpiga
marufuku mjumbe wa umoja huo,Kennedy Mpumilwa kutoshiriki kampeni za uchaguzi
mdogo wa ubunge wilayani humo.
Pia,uongozi
huo umemtaka Mpumilwa kutovaa sare za chama hicho huku wakimtuhumu ya kwamba amekuwa
akikivuruga chama cha CCM wilayani humo kwa kutumiwa na wapinzani hususani
Chadema.
“Kennedy
siku zote amekuwa mjenga hoja wa kubomoa hoja za CCM Arumeru,asionekane amevaa sare
za CCM na wala asishiriki kampeni za CCM wakati mchakato utakapoanza”alisema
Pallangyo ambaye ni mwenyekiti wa Uvccm kata ya King”ori wilayani Arumeru
Katika kikao
hicho waliohudhuria ni mwenyekiti wa Uvccm mkoa wa Arusha,James Ole Millya,mwenyekiti
wa Uvccm wilaya ya Arumeru,Esther Maleko pamoja na wenyeviti 17 wa Uvccm wa
kata 17 za wilayani humo.
Tamko hili
limefuatia baada ya Mpumilwa ambaye ni mjumbe
wa baraza la vijana mkoani Arusha kupinga vikali matokeo ya uchaguzi wa
kumtafuta mwakilishi atakayepeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi wa ubunge
wilayani humo mtoto wa marehemu Sumari,Sioi
Sumari kwa madai kwamba ulijaa rushwa.
Akitoa tamko
hilo jana katika ofisi za CCM zilizopo eneo la Kikatiti wilayani humo kwa niaba
ya wenyeviti 17 wa kata wa Uvccm wilayani Arumeru aliokuwa ameambatana
nao mwenyekiti wa Uvccm kata ya King”ori,Pallangyo alisema kwamba taarifa zinazotolewa na baadhi ya vyombo vya
habari kwamba hali si shwari ndani ya jumuiya yao si za kweli.
Pallangyo,alisema
kwamba mara baada ya uchaguzi wa awali wa kumpata mgombea atakayepeperusha bendera
ya CCM kumekuwa na taarifa kwamba hali
ya kisiasa ndani ya umoja wao si shwari kwa kuwa kuna mgawanyiko kitendo
ambacho alidai kinapotoshwa na watu wachache.
Alisema
kwamba kumekuwa na taarifa ambazo zimekuwa zikitolewa na Mpumilwa kwamba
uchaguzi huo ulijaa rushwa na mizengwe kitendo ambacho si sahihi huku
akisisitiza kwamba kada huyo ametumwa
kuvuruga umoja na chama chao na wapinzani.
Alimtuhumu
kada huyo ya kwamba mara kwa mara amekuwa akijichukulia madaraka wakati si yake
kwa kutoa matamko mbalimbali wakati yeye si msemaji wa chama wala jumuiya ya
vijana wa chama hicho wilayani Arumeru.
“Ifahamike
ya kwamba msemaji wa jumuiya yetu ni mwenyekiti,katibu na katibu
hamasa,Mpumilwa sio msemaji wa chama siku zote amekuwa akijichukulia madaraka
wakati si yake”alisisitiza Pallangyo
Hatahivyo,aliutaka
uongozi wa CCM ngazi ya mkoa na taifa kwa ujumla kumwajibisha Mpumilwa kwa kumchukulia
hatua za kinidhamu kwa mujibu wa katiba ya CCM kwa kuwa amekuwa amekiuka
maadili ya chama hicho.
Wakati huo
huo,Milya ndani ya kikao hicho alijitapa kwamba chama chao kina uhakika wa
kushinda uchaguzi katika jimbo la Arumeru Mashariki huku akisema kwa mafumbo kwamba
hata katika harusi mbalimbali nchini wamekuwa wakiingia watu walioalikwa na wale
wazamiaji.
Bila
kuwataja wazamiaji na waalikwa ni wakina nani Milya alisema kwamba Uvccm imejipanga
kikamilifu kupambana kwa lengo la kunyakua jimbo hilo kwa kuwa wanajiamini
watashinda.
Hatahivyo,Mpumilwa
amekaririwa na vyombo mbalimbali vya habari akijibu mapigo kuhusina na tamko
hilo la umoja huo huku akisema ya kwamba hatishiki kwa kuwa kikao kilichofanyika
sio halali kwani hata yeye hakuitwa
kupewa nafasi ya kujibu madai yake.