WANASIASA wa mkoa wa Arusha
wametakiwa kuacha malumbano na kusema kuwa hawatambuani kwani hali hiyo
inachangia kwa kiwango kikubwa sana
kuongezeka kwa umaskini na jamii kukosa haki zake za msingi ambazo ndizo chanzo
pekee cha lkuwachagua Viongozi.
Hayo yamebainishwa mjini na
mwenyekiti wa chama cha kijamii (CCK) bw James Ndarivoi wakati akiongea na
waandishi wa hahabri kuhusiana na migogoro ambayo inaendelea ndani ya mji wa
arusha baina ya wanasiasa.
Bw Ndarivoi alisema kuwa wapo baadhi ya watendaji wa Serikali
hususani kwenye halmashauri ya Jiji ambao wananufaika na mgogoro huo baina ya
wanasiasa kwa kuwa Viongozi mbalimbali ndani ya jiji la Arusha hawatembelei
Manispaa ya jiji kwa ajili ya itikadi za kisiasa.
Aliongeza kuwa hali hiyo ina
matatizo makubwa sana
na Viongozi wanashindwa kukumbuka ahadi ambayo waliitoa kwa wananchi hali
ambayo inasababisha walengwa kukosa haki zao za msingi.
‘ukiangalia utaweza kuona
kitu kinachoendelea jijini hapa kwa sababu mwanasiasa anadiriki kusema kuwa
hamtambui kiongozi mwingine na kwa hali
hiyo hata baadhi ya watu ambao hawana maadili wanatumia nafasi hiyo kujinufaisha
kwa kuwa hawana mtu wa kuwauliza”alisema Bw Ndarivoi.
Pia aliongeza kuwa nao
viongozi wa jiji la Arusha wanatakiwa kujua na kutambua kuwa wamechaguliwa na
wananchi kwa hali hiyo basi wanatakiwa kujikita zaidi kwenye maendeleo na wala
sio malumbano ya kisiasa
Alibainisha kuwa endapo kama wataendelea na malumbano ambayo yanazaaa kesi za
mahakama kila mara ni wazi kuwa Jiji litaendelea kukabiliwa na changamoto
lukuki kutokana na kukosa ushirikiano wa kijamii.
Katika hatua nyingine bw
Ndarivoi alisema kuwa wao kama cha kijamii wanatarajia kufanya mabadiliko
makubwa sana
kwa jiji la Arusha ikiwa ni pamoja na kubadilisha na kuimarisha zaidi
miundombinu
Alisema kuwa wanatarajia
kutumia Katiba mbalimbali za maendeleo ambapo Katiba hizo zitaweza kuleta
mabadiliko mbalimbali tofauti na sasa ambapo jiji linakabiliwa na changamoto
kubwa sana.