Viongozi wa serikali wamaaswa
kuthibiti wafanyakazi wa fani ya hotelia wanaoingia nchini kutoka nchi jirani
ili wazawa waweze kupata nafasi za ajira kwa kuwa wanauwezo wa kufanya kazi
kikamilifu na ubora unaotakiwa.
Hatua hiyo inafuatiwa na
wimbi kubwa la wafanyakazi wa fani hiyo kujaa katika mahoteli hapa jijini
arusha hali ambayo inapelekea watanzania kukosa ajira katika sekta hiyo huku
wakiwa na elimu na sifa zinazofanana.
Meneja msaidizi wa hoteli ya
Naura spring iliyopo jijini hapa bw.Robert Antony
amesema hayo wakati wa mahafali ya pili ya chuo cha Eureka
wakati wa alipokuwa mgeni rasmi ambapo amedai kuwa tatizo hilo linazidi kuongezeka na hakuna hatua
iliyochukuliwa hali ambayo itahatarisha ajira za watanzania waliosomea taaluma
hiyo.
Antony ameongeza kuwa wakati umefikia sasa vingozi wa
serikali wenye mamlaka husika kukemea tabia hiyo kwa kuwa kuna vijana
wengi wenye uzoefu na taaluma hiyo ya
kutosha lakini wamekuwa hawapewi ajira hali ambayo in apelekea tatizo la ajira
kuongezeka zaidi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa
bodi ya chuo cha EUREKA Beatrice Assenga
amewaomba wadau wote na jamii kwa ujumla kuwawezesha wanafunzi wenye uwezo
kitaalauma kwani ni nguvuu kazi ya taifa.
Beatrice amesema kuwa ikiwa
kama taasisi na sekta zote za ajira hapa nchini zitaamini na kuthamini elimu na
ujuzi wa kijana wa kitanzania kwa misingi ya kithibitisho wa ufaulu pasipo
kuweka pingamizi la uzoefu kazini basi
ni wazi vijana wengi watapata ajira na tatizo la vijana kukosa kazi litakuwa
limepungua kwa kiasi Fulani.
Pia amewaomba wamiliki wa
mahoteli jijini Arusha na taasisi mbalimbali kutowatoza ada wanafunzi wakati wa
mazoezi ya nje kwa vitendo kwani ni ianaleta wanafunzi usumbufu.
Amesema
kuwa wanafunzi wanapata adha kubwa kwa kuwa wengi wanaotoka katika
familia zenye uwezo wa hali ya chini na wanashindwa kumudu.