mwanafunzi wa kidato cha pili
katika shule ya sekondari ya Arusha day,mkazi wa Olmatejoo,Emanuel Agrey(15)amejinyonga
kwa kutumia kitenge cha mama yake mzazi hadi
kufa kwenye kamba ya kuanikia nguo.
Kamanda Andengenye alifafanua kuwa tukio hilo
limetokea jana majira ya saa 10 jioni katika eneo la Olmatejoo ,ambapo mama
mazazi wa marehemu huyo,Magreth Stewart (37) aliukuta mwili wa mtoto wake ukiwa
umening’inia kwenye kamba hiyo ya kuwanikia nguo alipokuwa akitoka kanisani.
Alisema kuwa mama huyo baada ya kuona mwili huo
alitoa taarifa kwa watu mbalimbali akiwemo mume wake,Agrey Stewart ambapo kwa pamoja waliingia ndani na
kushuhudia tukio hilo na baadae walitooa taarifa kituo cha polisi ,ambao askari polisi walifika na kuondoka na mwili
huo.
Kwa mujibu wa kamanda Andengenye chanzo cha tukio
hilo bado hakijajulikana na kwamba polisi wanachunguza tukio hilo huku na mwili
wa mwanafunzi huyo ukiwa umehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospitali
ya mkoa mount Meru.