Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (SACP) Thobias Andengenye akitoa shukrani kwa Kampuni ya Vodacom wakati wa hafla ya makabidhiano ya kituo cha Mto wa Mbu kilichopo wilayani Monduli siku ya Alhamisi.Kushoto kwake ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom nchini Bi. Mwamvita Makamba na Mkuu wa kampuni hiyo Kanda ya Kaskazini Bw.Nguvu Kamando
.Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Arusha ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo (SACP) Thobias Andengenye akipanda mti wa ukumbusho katika kituo cha Polisi Mto wa Mbu kilichopo wilayani Monduli mkoani hapa
Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Kampuni ya simu za mkononi ya vodacom nchini Mwamvita Makamba akipanda mti katika kituo cha Mto wa Mbu kilichopo wilayani Moduli ikiwa ni sehemu ya ukumbusho na utunzaji wa Mazingira
Jeshi la polisi nchini kupitia mkuu wa jeshi hilo inspekta jenerali Said Mwema limeishukuru kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kwa kukarabati kituo cha polisi cha mto wa mbu wilayani Monduli.
Akitoa shukurani kwa Kampuni hiyo katika hafla fupi ya kukabidhi kamanda wa polisi mkoani hapa Thobias Andengenye alisema kuwa jeshi hilo kupitia kwa Inspekta jenerali said Ally Mwema wanaishukuru kampuni hiyo kwani katika kipindi hiki wanahitaji msaada wao wa hali na mali katika kulisaidia jeshi hilo linalo kabiliwa na uhaba wa vituo na uchakavu wa vituo vingi na kuwa ni kuthamini na kuimarisha ulinzi wa mali za raia na kuwa si kwa jeshi la polisi pekee ni wa wananchi wa weneo husika.
Kamanda Andengenye alisema anaamini kuwa wananchi wa eneo hilo wamefarijika kwa kusogezewa huduma za kipolisi karibu yao na kuwa wataipenda kampuni hiyo kwa kuwajali wao na mali zao na kuwa jeshi hilo mkoani hapa litakuwa tayari kutoa msaada wa kiusalama wakati wowote kwa kampuni hiyo na kuwa kuanzisha huduma ya M-PESA kumepunguza wimbi la uhalifu.
Ambalo lilikuwa linatokana na wananchi kutembea na fedha taslim na alipenda huduma hiyo kuboreshwa zaidi ilikuendelea kutokomeza uhalifu nakuwataka kutotembea na fedha mikononi wakati wakienda kununua bidhaa madukani, pia aliwaahidi wananchi wa mto wa mbu kurudi kulizungumzia suala la ulinzi shirikishi na kero mbali mbali jambo litakalosaidia mahusiano ya jeshi hilo na wananchi.
Nae mkuu wa kampuni hiyo kanda ya kaskazini Nguvu Kamando alisema wao kama kampuni ya mawasiliano hawnabudi kusaidia jamii kama sehemu ya wateja na kampuni ya Vodacom inatambua mchango wa jeshi la polisi katika kulinda usalama wa wateja wao na mali zao hali hiyo ndiyo inayowawezesha kutekeleza majukumu yao na kuwa huduma ya M-PESA ikitumiwa vizuri inaweza kuwa mkombozi wa wananchi katika kuinua kipato na uchumiu kwa ujumla
Alisema Kamando kuwa ukarabati wa kituo hicho ulianza mwaka jana kwa kukarabati chumba cha mahabusu,chumba cha kutunzia silaha,ofisi ya OC-SS,na chumba cha mashtaka na umegharimu kiasi cha tsh.17 milion,sherehe hizo mbali na mgeni rasmi pia alikuwa meneja uhusiano na masoko wa kampuni hiyo bi Mwamvita Makamba ambao yeye na mgeni rasmi walipanda miti ya ukumbusho wa makabidhiano hayo na utunzaji wa mazingira.kituo hicho kina hadhi ya daraja”C”