SHIRIKA
la Compassion Tanzania limeonyesha nia ya kupunguza adha ya upatikanaji wa maji
safi hususani nyakati za kiangazi kwa kutoa msaada wa visima vitatu kupitia
mradi wa uvunaji wa maji ya mvua uliotolewa kwa ajili ya huduma watoto zaidi ya
280 waliopo mjini Kibaya wilayani Kiteto mkoani Manyara.
Kwa
mujibu wa mkurugenzi mkuu wa shirika hilo mchungaji Joseph Mayalla ambalo
kwasasa limeweza kutoa huduma ya elimu ya awali,ufundi stadi hadi vyuo vikuu
kupitia huduma ya afya kwa mtoto kwa watoto 65,000 waliopo kwenye mikoa 12
nchini amesema msaada huo uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 32,licha ya
kuwalenga watoto wa mji huo lakini pia utainufaisha jamii ya mji wa Kibaya
yalipo makao makuu ya wilaya hiyo.
Aidha
mchungaji Mayalla ameongeza kuwa katika kuhakikisha shirika hilo linatoa huduma
ya afya lakini pia litahakikisha kuendelea kuwasaidia watoto walio katika
mazingira magumu ili kutimiza malengo yake hadi 2020 bila ya kujali itikadi za
kidini ili kupunguza umaskini,ujinga na maradhi na kuisaidia serikali kwa
wananchi wake.
“lazima
tuwe na mkakati tunataka tuwe na kizazi sio cha wanung’unikaji na walalamikaji
tunataka tuwe na kizazi chenye kutafuta suluhisho ufumbuzi wa matatizo badala
ya kukaa kwenye magenge ya walalamikaji..tunataka kizazi kinachojiuliza
tutaifanyia nini Tanzania na sio Tanzania itatufanyia nini hayo ndio malengo
yetu ya milenia”
kwa upande mwingine licha ya kuhimiza familia
kubuni hifadhi za maji ya mvua ili kuondokana na magonjwa ya milipuko ameitaka
jamii kupanda miti ili kuiunga serikali katika kampeni zake za kupunguza hewa
ya ukaa ambayo tayari imeonyesha kuleta madhara makubwa ya uharibifu wa
mazingira na mmomonyoko wa ardhi.
Akizindua
mradi huo kwa niaba ya mkuu wa wilaya katibu tawala wa wilaya hiyo Fidelisi
Kyoro amelipongeza shirika hilo kuunga mkono ilani ya serikali iliyopo madarakani
kwa kupunguza adha ya tatizo la maji lililopo katika mji huo yalipo makao makuu
ya wilaya hiyo ambalo amesema ni kubwa na linalotakiwa kutafutiwa ufumbuzi.
“tunategemea
mabwawa yanayochimbwa kwa kutegemea mabwawa ya DADPS na yale ya asili,tunategemea
visima virefu vinavyochimbwa na serikali ama wafadhili tunategemea tatizo kubwa
hatuna vyanzo vingi vya maji na mito wilayani kwetu”
Aidha Kyoro
alisema kutokana na tatizo hilo kupitia jitihada za serikali kwa kushirikiana
na mashirika ya kitaifa kama vile benki ya dunia ambayo imejaribu kuchimba
visima 14 lakini kati ya hivyo ni saba tu yaliyoonyesha mwelekeo ya upatikaji
wa maji endelevu toka kwenye kina cha futi 200.
“hapa kwa
visima vifupi huwezi kuchimba na kupata maji mpaka uchimbe visima kirefu
ambacho kinagharimu fedha nyingi hadi milioni 30,hilo ni kazi kubwa lakini kama
mnavyofanya sasa watu wetu wanaelimishwa kutafuta mbinu ya kuvuna maji ya mvua
ambapo tumeanza sasa”
Hata
hivyo kwa upande mwingine baadhi ya wanawake wa mji huo wakishukuru kuwepo kwa
visima hivyo amesema utatoa nafasi kwa wananchi kujifunza na kuepukana na
magonjwa ya milipuko kama vile kipindupindu yanayosababsihwa na matumizi ya
maji ya visima yasiyokuwa salama.
“kero ya
maji wilaya ya kiteto ni kubwa saana..hata mradi wa halmashauri wamekuwa
wakipandisha gharama kila wakati leo shilingi mia kesho zaidi inamaana kuna
kero kubwa ya maji,hata mradi wa maji umekuwa kama wa binafsi kutokana na
upandishwaji wa maji kiholela”alisema bi zena ndaro.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia