BREAKING NEWS

Tuesday, March 13, 2012

FOMU YA UCHAGUZI NAMBA 17 INATUMIKA KWA VIGEZO TU

Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Arumeru Mashariki Transias Kagenzi
 
 
 kutokana na sheria ya uchaguzi  sura  namba 343   mtu yeyote hataruhusiwa kupiga kura bila ya kuwa na kitambulisho cha mpiga kura.

Hayo yamebainishwa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Arumeru mashariki Trasias Kagenzi wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru ambao unatarajiwa kufanyika Aprili moja mwaka huu.

Alibainisha kuwa kuna maombi ambayo wameyapata kutoka kwa vyama  wakidai kuwa wanataka wanataka kutumia form namba 17  ambayo inamruhusu mwananchi kupiga kura iwapo amejiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura.

Alifafanua kuwa kutoka na kifungu cha sheria sura namba 343  kinadai kuwa mtu yeyote ambaye amejiandikisha kupiga kura hataruhusiwa kupiga kura iwapo hana kitambulisho cha kupigia kura ila mtu huyo ataruhusiwa kutumia fomul hiyo namba 17 iwapo tu  atakuwa amejiandikisha na kitambulisho chake kipo ila kinamashaka .

"sheria hii inaruhusu tu mtu ambeye amekuja kupiga kura lakini kitambulisho chake kina mashaka  nikimaanisha hakieleweki ,kimechanika au msimamizi wa  anakuwa na hofu na kitambulisho hicho hivyo tunamruhusu atumie fumu hii namba 17 ili iwapo atakuwa anatudanganya achukuliwe sheria hivyo kama mtu hana vigezo hivi hatutaweza kumruhusu apige kura "alisema Kagenzi.

Alibainisha kuwa mpaka sasa tume imejipanga vyema katika uchaguzi na  tume imeingia jimbo hili la Arumeru na itakuwa hapa hadi pale uchaguzi takapo kamilika.

Aidha alibainisha kuwa kwa kipindi hichi wameboresha mambo mengi  na vifaa vimeshandaliwa pamoja na vituo vyote vya kupigia kura ambapo alibainisha kuwa kutakuwa na jumla ya vituo 327 vya kupiga kura  ambavyo vyote vimejulikana na vimeandaliwa.

Aliongeza kuwa kuna baadhi ya watu ambao walikuwa wanadai kuwa vitambulisho vyao vya kupigia kura vipo kwa Ocd na wao wameshatoa taarifa kwa ocd kutoa vitambulisho hivyo vya kupigia kura kama vipi kwake avirejeshe kwa wananchi lakini ocd amewajibu kuwa hada kitambulisho cha mtu yeyote cha kupigia kura.

"napenda kuwaambia wananchi kama anakitambulisho chake kwa ocd kituo chochote chaq polisi akakichukuwe mapema na kwa sasa hivi katika kipindi hichi cha kampeni tumezuia mtu yeyote kumwekea mthamana mtu kwa kutumia kitambulisha cha kupigia kura hivyo pia napenda kuwasihi viongozi wa vyama wawaambie wafuasi wao wakachukue vitambulisho vyao katika vituo vya polisi iwapo wanatakuwa waliekea mtu mthamana na ajakichukuwa ili aweze kumpiga kura''alisema Kagenzi.

Alisema kuwa  wasimamizi wa uchaguzi wapo magari wanayoyakutosha  ,karani waongoziaji pia wapo ,pamoja na askari wa kulinda vituo vyote vya kupigia kura na kwakipindi hichi wameboresha zaidi kwani askari watakao linda ni askari polisi na sio mgambo kama ilivyozoeleka.

Kagenzi alisema kuwa katika tatizo la kutangaza matokeo kwa muda muafaka halitakuwepo kwani tume imeboresha vifaa ikiwa ni pamoja na kuleta komputa kwa kwa ajili ya kuhesabia matokeo ,na alibainisha kuwa kutakuwa na komputa nyingi ambazo zitasaidia na kusema kuwa tume wenyewe watakuwa na komputa saba huku yeye kama msimamizi atakuwa na komputa nane.

Aliwataka watu wajitokeze kuhakiki majina yao kwenye dafutari la mpiga kura iwapo tu watasikia tangazo na alisema kuwa wanampango wa kubandika majina hayo siku nane kabla ya uchaguzi kufanyika.

Kagenzi  aliwataka viongozi mbalimbali wa dini yakiwemo makanisa na misikiti kuwahimiza wananchi wao kwenda kusikiliza kampeni na sera za wagombea huku akitoa onyo kwa viongozi hao kuto wapigia kampeni  wagombea wala kuwahimiza wananchi kumchagua mgombea fulani

Katika jimbo hili la Arumeru Mashariki kuna jumla ya wapiga kura 127247 pamoja na vituo vya kupigia kura 327.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates