TLP YAZINDUA KAMPENI ZA LEO TENGERU

Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustino Mrema ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo,   anahutubia katika kiwanja cha  Tengeru  hii ikiwakihutubiaa ni uzinduzi wa kampeni za chama hicho
Mwenyekiri wa TLP akiwa anamnadi mgombea ubunge wa chama hicho Alexzanda Abrahamu katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho


Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustino Mrema ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo amewataka wananchi wa jimbo la Arumeru Mashariki kuchagua kiongozi mchapa kazi na sio kiongozi anayetumia hela kupata nafasi ya ubunge.

hayo hameyasema leo wakati akizindua kampeni za uchaguzi za chama chake katika uwanja wa Patandi uliopo tengeru ambapo pia alichukuwa nafasi hiyo kwa ajili ya kumnadi mgombea wa chama chake .

Alisema kuwa  ni nafasi ya kila mwananchi wa jimbo la Arumeru mashariki kuchagua kiongozi machapa kazi ambaye ataliletea jimbo hilo maendeleo na sio kuchagua kiongozi mradi amemchagua kwa kudanganywa na vizawadi vidogo vidogo ikiwemo kofia ,tisheti pamoja na vinywaji  mbalimbali.

'' mimi napenda kuwasihi kuwasihi wana wa Arumeru kutowashabikia watu wenye ela ,helkopta na magari lakini hawawasaidii kwani watapita mtawashabikia na badala yake watawaacha mkiwa na shida zetu bora mchague chama changu kwani mimi pia nilishawasaidia na kinanishangaza zaidi nakuja kuomba kura mnaniuliza helkopta ikowapi mimi nawauliza mbona nilivyokuja kuwapatanisha hamkuniuliza hivyo kwa iyo kuweni makini sana katika uchaguzi huu''Alisema Mrema

Aidha alisema kuwa wasishabikie viongozi wanaozuka na wasiokuwa na histori  bali wachague viongozi ambaye anajulikana historia yake na ambaye anaeza kutetea kweli  matatizo yao na kuwafumbulia matatizo yao .

Aliwaomba wananchi wao wamsaidie kumpitisha mgombea wa chama hicho  kama jinsi yeye alivyowasaidia kuwasuluisha katika kipindi cha mgogoro wa kanisa uliotokea mwaka 1993 mgogoro ambao maaskofu walishindwa kuutatua ,viongozi wakubwa walishindwa kuutatua hadi pale yeye alipoenda  na kuupatia ufumbuzi.

''Mnajua bibilia inasema hivi mtoto akimuomba baba yake samaki atampa nyoka ,na je mtoto akimuomba baba yake mkate atampa ng'e sasa mimi ni mtoto nimekuja kuwaomba mumsaidie mgombea wangu nataka nione kama mtanipa nyoka ama jiwe''alisema Mrema

Aliwaambia wananchi kuwa iwapo mgombea wake atapewa kura na kushinda basi atashirikiana naye kuhakikisha shuhuli za maendeleo zinafanyika ukizingatia yeye yupo kwenye ukaguzi wa fedha za serekali na kubainisha kuwa kitu cha kwanza kufanya ni kumleta mkaguzi mkuu wa hesabu za serekali ili akague miradi yote iliyopo katika jimbo hilo na endapo watakuta kunaubadhilifu wa aina yeyote basi atachukuliwa sheria.

Alitoa  wito wa viongozi wa dini ikiwemo wachungaji ,maaskofu pamoja na wazee wa mila kumsaidia kupiga kampeni ili ashinde kama jinsi yeye alivyowasaidia kuwapatanisha kipindi cha vita.

kwa upande wake mgombea ubunge wa chama hicho Alexanda Abrahamu alisema kuwa yeye akiwa kama mgombea aliamua kwenda kugombea nafasi hii mara baada ya kuobwa na wazee wa mila zaidi ya 200 ambao walienda kwake na kuomba agombee ili aweze kusaidia ubunge wa kurithiana usiwepo jimboni hapo.

Aidha mwenyekiti huyu aliilalamikia ratiba ya mikutano ya adhara ambayo wamepangiwa huku akisema kuwa ratiba hiyo aieleweki na inawachanganya na kuwasababisha hasara.

''mimi wazee walinifuata na kunitaka nikagombee kwani walisema kuwa kunadalili za ubunge wa kurisishana umeingia jimboni hapo huku akidai kuwa mara baada ya kuombwa nawazee akashauriana na mwenyekiti wa chama chao TLP na kuamua kuja kugombea na nachopenda kuwaambia wana arumeru mashariki msikubali kutoa kura zenu wala kutawaliwa na ubunge wa kurisishana kama wafalme''alisema Alexanda

Alibainisha kuwa iwapo wananchi wa Arumeru watampa nafasi ya uongozi atahakikisha tatizo la maji linaondoka na pia atawasaidia kulinda aridhi yao ambao imechukuliwa na mafisadi pamoja nakusaidia kuwapa ajira vijana wao wengi ambao wapo mitaani bila ajira.

Alitoa wito kwa wananchi kujiandaa vyema kwenda kupiga kura huku wakichagua kiongozi ambae anaweza kuwatatulia shida zao.


Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post