Kikongwe anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 96 mkazi wa mkaoni
Kilimanjaro ambaye jina lake halikutambulika .akiwa amezungukwa na umati
mkubwa wa watu katika eneo la standi ya mabasi yaendeyo mikoani(Dar
Express),baada ya kudaiwa kuanguka kwenye ungo usiku wa manane
wakielekea kushiriki masuala
ya ushirikina,katika eneo la makao mapya
KIKONGWE mwenye umri unaokadiliwa kuwa na miaka 96 ,mkazi
wa kibosho mkoani Kilimanjaro ,amezua tafrani kubwa jijini Arusha baada ya
kukutwa akiwa uchi wa mnyama akidaiwa kuanguka ghafla usiku wakati akisafiri kishirikina kwa kutumia
ungo .
Kikongwe huyo ambaye jina lake halikutambulika mara moja
,alionekana akiongea lugha ya kichaga pekee kwa taabu ,na mara nyingi alikuwa akipoteza
kumbumbu pindi anapohojiwa ili kutambua mahala alipotoka na anakoelekea.
Kwa mujibu wa mashuhuda wamedai ya kuwa kikongwe huyo
alionekana katika kituo cha mabasi cha Dar Express majira ya saa kumi usiku
akiwa hana nguo,na kwamba alionekana akianguka ghafla kutoka angani katika
mazingira ya kichawi.
Wameeza kuwa baada kumkuta katika hali hiyo ya utupu
baadhi ya wasamalia walimwonea huruma na kumpatia nguo ya kujisitili, hata
hivyo mudfa mwingi kikongwe huyo alishindwa kueleza ni jisi gani amefika hapo.
Aidha wamebainisha kuwa pamoja na watu mblimbali wa kabila la kichaga
kufika na kujaribu kuongea nae ili kujua yaliyomfika ,alishindwa kuongea na
kusikika akiongea kwa taabu bila maneno yake kueleweka hali ambayo ilisababisha
umati mkubwa wa watu kufurika na kumzunguka huku wengine wakitaka kumpiga
wakiamini kuwa alikuwa mchawi.
Kufuatia tukio hilo,polisi mjini Arusha walipata taarifa
na kufika eneo la tukio ambapo walifanikiwa kuondoka na kikongwe huyo hadi
kituo cha polisi mjini kati kwa mahojiano zaidi.
Hata hivyo mwandishi wa habari hizi akiondoka eneo la kituo cha polisi ,kikongwe
huyo alikuwabado hajaongea chochote ,huku polisi na watu mbalimbali walikuwa wakijaribu
kumhoji bibi huyo huku wanamaombio nao wakijaribu kumwombea.