Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amewasili mkoani Kilimanjaro apa alikuwa anasalimia na baadhi ya viongozi wa mkoa huo
wanawake wa mkoa wa Kilimanjaro walijitokeza kumpokea Rais huku kila mmoja akionekana akiwa na uso wa furaha
Raisi alipokelewa na vikundi vya ngoma za asili hapa alikuwa anaangalia wakicheza
Mwenyeji wa ugeni huu ambaye ni mkuu wa mkoa wa |Kilimanjaro Leonidas Gama akiwa anawapa wageni wake histori fupi ya mkoa
Miongoni
mwa shughuli ambazo Mheshimiwa Rais atafanya ni pamoja na kuzindua
kampeni ya kupinga ukatili na matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake ambayo
ataizindua kwa kuanzisha safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro iliyopewa
jina la “Kilimanjaro Speak Out, Climb Up”.
Shughuli
hiyo itakayofanyika leo Jumatatu, Machi 5, 2012 asubuhi, imepangwa
kwenye Lango la Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA)
Mbali
na kuanzisha kampeni hiyo, Mhe Rais pia atafungua Mkutano wa Mwaka wa
Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika kwenye Chuo cha Polisi
mjini Moshi.
Hii
ni ziara ya kwanza ya Mhe Rais Kikwete katika Mkoa wa Kilimanjaro tokea
alipotembelea Mkoa huo wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka
2010.