Mmoja wa wajumbe wa bodi mpya ya Kahawa walioteuliwa Meynard Swai ambaye pia ni Meneja wa KNCU.
Rais Jakaya Kikwete amemteua Bibi Eze Hawa Sumari
kuwa mwenyekiti mpya wa bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) kuchukua nafasi ya Pius
Ngenze.
Ngeze amekuwa mwenyekiti wa bodi hiyo tangu mwaka
2008 hadi Desemba mwaka jana ambapo bodi yake ilimaliza muda wake wa uongozi
Tayari Ngeze na wajumbe wengine waliomaliza muda
wao wameagwa rasmi na watumishi wa bodi hiyo katika hafla iliyofanyika February
27,2012
Sanjari na mwenyekiti huyo pia waziri wa
kilimo,chakula na ushirika Prof Jumanne Maghembe ameteua wajumbe wapya
watakaounda bodi hiyo.
Wajumbe hao ni pamoja na Fatuma Faraji ,Novatus
Piigererwa, Yasinti Ngwasura na Eric Ng'maryo.
Wengine ni Maynard Swai ambaye ni Meneja wa KNCU,Prof James Terri ambaye ni mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa zao la Kahawa(Tacri),Mh John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga na Eng Merad Omar Msuya.