mkuu wa wilaya ya Arumeru Mercy Sila akiwa anapanda mti katika kijiji
cha Kivuluvuli kijiji kiichopo wilayani Arumeru mkani Arusha sehemu
ambacho ndipo wiki ya maji imezinduliwa uko kwa mkoa wa Arusha
,alipanda mti huu kwa ishara ya kuonyesha ni jinsi gani wameweza
kuifadhi eneo hili kwa ajili ya maji
mwenyekiti wa bodi ya AUSA Filex Mrema akiwa anaweka mchanga kwenye
nguzo ambazo waliziotesha katika kiwanja hicho ambazo ni za uzio
uliozuia kupita
watu
mkuu wa wilaya ya Aruemeru mercy Sila akiwa anahutubia wananchi waliouthuria katika sherehe za uzinduzi wa wiki ya maji
kulikuwepo pia na ngoma ya mdumange
wamasai nao hawakuwa nyuma walijitokeza kutoa burudani
Serekali imetakiwa kuwachukulia hatua kali wale wote ambao
wanafanya kazi ya kukata miti bila vibali pamoja na wale wote ambao hawatunzi
mazingira ambayo yanawazunguka
Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa kijiji cha Kivululu
Raphael Kulei wakati alipokuwa
anangongea katika sherehe za uzinduzi wa wiki ya maji iliyozinduliwa katika
kijiji cha kivulili kilichopo katika kata ya Orturoto wilayani Aruemeru mkoani
hapa .
Alisema kuwa ni wajibu wa serekali kufuatilia kwa makini
watu ambao wanakata miti ovyo pamoja na wale wanaoaribu mazingira ili kuweza
kupunguza tatizo kubwa la maji ambalo ndilotatizo kubwa linaloikabili nchi yetu
kwa sasa na hata mkoa wetu kwa ujumla.
Alibainisha kuwa wao kama viongozi wa kijiji wamekuwa
wakipata tabu kubwa kwani wamekuwa wakiwakamata watu na kuwapeleka mahakamani
kwa ajili ya kuharibu mazingira lakini wamekuwa hawapewi ushirikiano wa kutosha
na idara zinazoshughulikia maliasili ambao ndio watu wakuu ambao wanaostaili
kulinda vyanzo vya maji.
“kwanza kabisa napenda kama itawezekana serekali itoe idhana
iliyowekwa kuwa kata mti mmoja panda miti kumi kwa sababu watu wamekuwa
wanakata miti na hawapandi na atakama wakipanda hawaifatilii kuhakikisha mti
ule unaendelea kukuwaje mbali na ivyo watu wamekuwa wanakata miti bila vibali
na iwapo serekali ya kijiji itamkamata mtu Yule na kumchukulia hatua za kisheria basi mtu Yule ataendesha
ile kesi na ikifika huko mbale anaingiza siasa na kesi ile unakuta inaisha bila
sababu na navyo ona tukiendelea na tabia hii
nchi yetu itazidi kuwa kama na ata itafikia mahali tutakosa hadi maji ya
kunywa “alisema kulei
Nae mgeni rasmi wa uzinduzi huu huu wa siku ya maji ambaye
ni mkuu wa wilayani ya Arumeru mercy Sila alisema aliwaambiwa wananchi wa
Arumeru kuwa siku hii ni muhimu sana
kwani maadhimisho haya yamefanyika arumeru sehemu ambayo ndio chanz kikubnwa
cha maji na ndio sehemu ambayo mkoa wa
Arusha unategemea maji kutoka wilayani hapo.
Alisema kuwa kwakuwa wao ndio watu wanaowapa wanchi wa
arusha maji basi wajitaidi kuifadhi maji ili wananchi wengine wasipate shida ya
maji ,alisema kuwa kama tunataka kutimiza dhana ya kilimo kwanza lazima tuwe na
maji na alibainisha kuwa ni wajibu wa kila mmoja kutunza maji yote na sehemu
zote ambazo maji yamepotea ni wajibu wa kutafuta njia ya kuyarudisha maji yale
kwa kuotesha uoto wa asili.
Alisema kuwa ni wajibu wa kila mtu kuzingatia sheria ya
mazingira ,sheria ya maji na sheria ya Aridhi kamakwamba sehemu zote za maji
tusiziguse na tufuate sheria ya kujenga umbali wa kilometa kumi kutoka katika
chanzo cha maji na iwapo tutatekeleza basi tatizo la maji litaondoka.
Alimtaka kila mtu
atafakari kauli mbiu ya mwaka huu ya maji inayosema kuwa maji ni usalama wa
chakula na aifanyie kazi huku akiwasihi
kila mtu ajitaidi kupanda miti katika kila sehemu ambayo anaishi na akiupanda
asiuache bali aufatilie kwa matunzo hadi pale utakapo kuwa.
Alisema kuwa serekali inadhamini sana swala la kutunza
mazingira na pia alibainisha kuwa zaidi ya kupanda mitipia tujitaidi kujenga
nyumba zetu kwa kufaata sheria tuachene na ujenzi holela holela na tusimamie
sheria tulizo nazo maelekezo tunayopewa na hatimaye tuweze kutunza mazingira.
“nachukuwa nafasi hii kuwaambia wananchi wa kivululu pamoja
na wananchi wa Arumeru kuhakikish akila mahali mti unaonekana pia napenda
kuwaambia tuweke mazingira yetu mazuri ili atimae kama mkoa tuweze kufanikiwa
na vyanzo hivi”alisema Silla
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia