IMEGUNDULIKA KUWA
nusu ya wanawake wajawazito kwenye kata ya masama wilayani hai mkoani
Kilimanjaro wanajifungulia majumbani au kwa wakunga wa jadi kutokana na
kukosekana kwa vituo vya afya katika kata hiyona kuathili maisha ya
wakazi hao .
Hali hiyo imesababisha idadi kubwa ya wanawake wa kata
hiyo kupoteza maisha kwani ni asilimia tatu tu ya wanawake hao ndiyo
wanajifungulia katika vituo vya afya idadi ambayo ni ndogo ukilinganisha na
hali halisi ya malengo ya milenia yenye kauli ya afya bora kwa kila mwananchi.
Wakiongea kwenye mkutano uliyohusisha wakazi wa vijiji
vya Mungushi,Kware,na kwa Sadalla,vya kata ya Masama kusini wilayani hai
uliyoandaliwa na shirika la kijerumani linalojihusisha na idadi ya watu duniani
DSW wakazi hao walisema kuwa vijiji hivyo vyote vinategemea zahanati moja tu
iliyopo kijiji cha kware ambayo haina huduma ya mama na mtoto.
Wakazi hao walisema kuwa zahati hiyo haina mhudumu wa
afya ya uzazi kwa zaidi ya miaka kumi na mitano baada ya aliyekuwa mhudumu wake
kufariki dunia hali ambayo inawafanya wanawake wenye ujauzito kukosa huduma
hiyo huku wakihuzunishwa na kauli chafu za wahudumu na ukosefu wa dawa ambao
umekuwa ni tatizo sugu katika vituo vya afya.
Walidai kuwa kata hiyo inazaidi ya watu 11,000 wanaotegemea
kituo hicho ambacho hakikidhi mahitaji ya wakazi hao wenye kukabiliwa na
magonjwa mbalimbali ambayo hayana ufumbuzi kwa sasa .
Afisa mtetezi wa shirika la DSW Diana Shuma alisema
kuwa baada ya kufanya uchunguzi wa kitaalumu na kugundua mapungufu hayo shirika
hilo liliamua
kuanzisha mradi wa heathy action wenye lengo la kuibua changamoto ,kujadili
maoni ya wananchi na kuweka malengo kisha kuwasilisha hoja hizo kwa watunga sera
ili kuyapatia ufumbuzi matatizo yanayohusu afya ambayo yamekuwa yakipoteza maisha ya watu wengi.
Diana alisema hadi sasa shirika hilo ilimefanikiwa kwa kiasi kukubwa kuwajengea
uwezo wananchi waishiyo vijijini kwenye wilaya mbalimbali hapa nchini lakini
juhudi bado zinahitajika ili kuzikwamua jamii hizo ambazo zimesahaulika na watoa
huduma kwa jamii ikiwemo serikali.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia