tulivyoingia kwenye mashindano haya tu tukakutana na bango hilo
aya sasa
tunadumisha mila bwana adi wenzetu wanaiga wanazipenda ngoma zetu
kulikuwa na burudani za ngoma mbalimbali apo ni wapiga ngoma wakionyesha uhodari wao
lazima nipate mpira nipishe mchezo huu unaitaji nguvu ya hali ya juu
wachezaji wa Rugby wakiwa uwanjani wana cheza
kocha wa timu ya taifa ya Rugby aliyevaa tisheti nyeupe akiwa anabadilishana mawazo na washiriki wa mashindano hayo na washabiki
Watoto wadogo wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki
katika mchezo wa Rugby ili mchezo huu
uwezo kukuwa zaidi na zaidi hapa nchini
Hayo yamebainishwa na kaputeni wa timu ya taifa ya mchezo
huo Bakari Shabani wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika
mashindano ya mchezo huo yaliyofanyika katika viwanja vya IMC mkoani hapa
alisema kuwa ni wajibu wa kila mtoto kushiriki mashindano haya kwani mashindano
haya yanafaida yake.
Alibainisha kuwa wazazi wamekuwa wakiwakiwakataza watoto wao
kushiriki mashindano haya wakidai kuwa mchezo huu ni wafujo kitu ambacho sio
cha kweli kwani mchezo huu ni mzuri kama michezo mingine .
Pia aliwataka wathamini mbalimbali wajitokeze kuthamini
mchezo huu ili vipaji vingi viweze kushiriki huku akibainisha kuwa mchezo huu
hautumii garama kubwa.
Kwa upande wake afisa
muandelezaji wa Rugby Tanzania Kittyler
Juma alisema kuwa wameandaa kuandaa mashindano haya ili kuweza
kuwahamasisha wazazi na watoto kushiriki mchezo huu.
Pia alisema wameshaanza kuhamasisha mashuleni kushiriki
michezo huu ambao unachezwa duniaa nzima
huku akibainisha kuwa kwa mkoa wa Arusha wameshatembelea shule mbalimbali
kuhamasisha na mpaka sasa kuna shule zimekubali na zinacheza mchezo huu.
“kunabaadhi ya shule zimekubali na zinacheza mchezo huu kwa
sasa na pia kunaambazo zinatuita ili tukafundishe mchezo huu katika shule zao
baadhi ya shule ambazo zinacheza mchezo huo na sasa ivi zipo katika mashindano
haya ni pamoja na st.Costanini ,Moshono,braiban pamoja na moshi intenation
schoo huku shule ya st. Jude ikiwa inatuita ili tukafundishe’’alisema juma.
Alibainisha kuwa
mpaka sasa wana timu mbalimbali zikiwemo timu za mchezo wa Rugby za
watoto wenye umri kuanzia miaka u-15 pamoja
na wale wenye umri chini ya miaka U-12 na pia wanafundisha watoto wadogo
ambao wanania na kuupenda mchezo huu.
“pia sisi tunafundisha watoto wanaopenda mchezo huu na kitu
tunachofanya kwa mtoto anaependa mchezo
huu ni kumlipia shule kwa kipindi chote atakacho kuwa anasoma ila shariti letu
ni moja tu mtoto awe anacheza mchezo huu wa ragibi”alisema Juma.
Alimalizia kwa kutoa wito kwa wazazi walezi na hata watoto
pia na vijana kujitokeza kushiriki mchezo huu kwani mchezo huu ni mzuri
unajenga mwili na kumfanya mtoto awena akili na uwezo wa kufikiria zaidi.
Alibainisha kuwa wathamini pekee ambao ndio wakuu
wamejitokeza kuthamini mashindano haya ni Hughes Mottors(T) Ltd ambao ndio
wamejitolea kusomesha watoto wote ambao watacheza mchezo huu na pia alitoa wito
kwa makampuni mbali mbali kujitokeza kuthamini mchezo huu akisema kuwa mchezo huu
ni sawa na michezo mingine .
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia