Mkurugenzi wa tume ya taifa Julias Malaba akiwa na kamati aliyoongozana nayo wakiongea na waandishi wa habari
Tume ya taifa ya uchaguzi
imetupilia mbali rufaa dhidi ya uamuzi wa msimamizi wa uchaguzi wa
kukataa pingamizi ya mgombea ubunge wa
chimbo la Arumeru mashariki Nassari Joshua
dhidi ya mgombea wa chama cha mapinduzi sumari sioi Solomon iliyokuwa ikidai
kuwa mgombea huyo sio raia wa Tanzania.
Akiongea mbele ya
waandishi wa habari mkurugenzi wa uchaguzi wa tume ya taifa Julias Malaba
alisema kuwa tume imeamua kutumbilia mbali rufaa hiyo kutokana na sheria ya
nchi yetu pamoja na yanchi ya Kenya ambayo inamuelezea raia wa Tanzania anatakiwa
awe na sifa gani.
Alisem a kuwa kutokana na pingamizi hizo ambayo imewekwa na
mrufani kwa msimamizi wa uchaguzi kuwa
mrufani si raia wa tanazania na alidai kuwa kwa mujibu wa sheria ibara ya
67(1)ya katiba ya jamuuri ya muungano wa Tanzania imedaiwa kuwa katika ibara ya
67(2) (a) ya katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania imekiukwa kwa vile
mrufani ana uraia wa nchi nyingine.
Akifafanua alisema kuwa swala hilo liliibuliwa kutokana na
mgombea wa chama cha mapinduzi na ilieleza kuwa mgombea huyo alizaliwa thika
nchini Kenya hivyo walidai kuwa kwa kuwa mgombea huyo alizaliwa nchini Kenya hivyo
alikuwa na uraia wanchi hiyo na kama sivyo angetakiwa kuukana uraia huo.
Alibainisha kuwa kutokana na malalamiko hayo tume iliamua
kupitia sheria ya uraia wa nchini Tanzania na walipopitia katika kifungu cha
5(2)cha sheria ya uraia ya Tanzania ya mwaka 1995 kifungu hicho kilieleza kuwa
mtu aliyezaliwa ndani ya jamuhuri ya muungano wa Yanzania wakati au baada ya
muungano na simstu aliyezaliwa nje ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania pia
alibainisha kuwa kwa mujibu wa kifungu cha sita cha sheria ya sita kinamtambua
mtu aliyezaliwa nje ya nchi huku wazazi wake wote wawili au mmoja akiwa raia wa
Tanzani akuwa ni raia wa kurithi toka kwa wazazi wake hivyo alibainisha kuwa
wao kama tume walipata maelezo kutoka kwa mrufani na kudai yeye alizaliwa
Nairobi nchini Kenya huku wazazi wake
wote wawili wakiwa raia wa kuzaliwa wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania hivyo
kwa mujibu wa uraia wa wazazi wake yeye ni raia wa kurithi kutoka kwa wazazi wake.
Pia alitumia kifungu cha sheria cha 7(1) ambacho
kinamzungumzia mtu yeyote aliye na uraia wan chi mbili ambapo alisema kuwa
pamoja na yeye kuzaliwa nchini Kenya hajawahi kuwa raia wa nchi ya Kenya na hivyo
hajawahi kuwa na urahia wan chi mbili ambapo alisema kuwa uraia wake ni wa nchi
ya Tanzania na auna utata kwa kuwa
aliandishwa na tume ya taifa ya uchaguzi
kuwa mpiga kura na kupatiwa kadi ya kupigia kura yenye namba 19627110 pia walisema
kuwa waziri wa mambo ya ndani anatambua uraia wake na alipatiwa hati ya
kusafiria (passport) yenye namba 179635 ambayo ilitolewa October 9 mwaka 2006.
Aidha alisema kuwa katika kifungucha 6 hakuna mahali popote
sheria inapomtaka mtu wa namna hii kuukana uraia wan chi moja pale atakapofikia
umri wa miaka kumi na nane hivyo mrufaniwa hakuwa na jukumu au wajibu au sababu ya kisheria ya kuukana uraia wowote
baada ya kufikia umri wa miaka kumi na nane.
Alisema kuwa hivyo tume ya uchaguzi katika kikao chake cha
machi 14 huu ilikaa na kujadili rufaa ya
mrufani na kuona kuwa suala kubwa lilikloibuliwa katika pingamizi na rufaa ya
mrufani ni kuhusiana na uraia wa mrufaniwa ameeleza katika fomu zake za mrufaniwa
katika fomu zake za uteuzi kwa yeye alizaliwa nchini kenye jijini Nairobi kitu
ambacho ni kweli lakini alibainisha kuwa mlalamikaji ajatoa kielelezo chochote
kilichoonyesha kuwa mrufani ni raia wa Kenya au alishakuwa raia wa Kenya .
“sisi tume hakuna popote ilipothibishwa kuwa mrufaniwa
alipaa uraia wa Kenya na kwa kuwa mrufani alipata uraia wa kenyea kuwa mrufani
ndiye aliyetoa madai kuwa mrufniwa alipata uraia wa Kenya kwa kuzaliwa nchini Kenya
basi alipaswa kuthibitisha madai yake kwa mujibu wa kanuni inayo sema he
whoalleges must prove his allegation”alisema
Mallaba
Alibainisha kuwa hivyo kutokana na sababu hizo tume ya taifa
ya uchaguzi imeridhika kabisa kuwa rufaa ya mrufani haina msingi hivyo
imetupilia mbali rufaa hiyo.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia