Mganga mkuu wa mkoa Frida Mokiti akiwa anachukuliwa kipimo cha damu kwa ajili ya kupima ugonjwa wa sukari
madaktari wakiwa wanafanya maandalizi kwa ajili ya upimaji
mganga mkuu wamkoa frida Mokiti akiwa anapimwa presha na daktari wa shirika la hifadhi ya jamii NSSF katika kiwanja cha sheikh Amri Abeid jijini Arusha huduma hii inatolewa bure kwa watu wote
Imebainika kuwa serekali imejielekeza zaidi katika kupambana
na magonjwa ya kuambukiza na kuyasahamu magonjwa siyokuwa ya kuambukiza kama
vile kisukari ,presha pamoja na Unene
Hayo yamebainishwa na Meneja Mafao wa matibabu wa shirika la
taifa la hifadhi ya jamii NSSF Dr.
Mtulia Alli wakati uzinduzi wa wiki ya shirika hilo ambapo kwa mwaka huu
wameanza kutoa huduma ya afya katika mikoa mbalimbali ukiwemo mbeya na hivi
sasa wapo mkoani hapa.
Alisema kuwa wao kama shirika la hifadhi ya jamii katika
uchunguzi wao wamebaini kuwa serekali kwa kipindi hichi imetelekeza magonjwa
yasiyo ya kuambukiza na kujielekeza zaidi katika magonjwa ya kuambukiza kama
vile ukimwi pamoja na kifua kikuu na
kuacha magonjwa ambayo ni sio yakuambukizana .
Alisema kuwa kutokana na kulemewa huko kwa serekali kwa
kuegemea sehemu moja hivyo shirika lao limeamua kuanza huduma hii ya mgonjwa
yasiyo ambakizwa ili kuweza kusaidia wananchi kutambua afya zao na kuweza
kuwapa morali ya kupima mara kwa mara.
Alisema wao kama shirika lengo lao kuu la kuanzisha huduma
hii ya upimaji bure kwa wananchi ni pamoja na kusaidia juhudi za serekali
katika utoaji huduma ya afya aswa katika magonjwa haya yasiyo kuwa ya
kuambukiza.
Alisema kuwa zoezi hili wanalifanya wao kama wadhamini wakuu
NSSF kwakushirikiana na watoa huduma binafsi (APHTFA) na wanampango wa
kutembelea mikoa mitano na huu ni mkoa wao wa pili kutoa huduma walianza na
mkoa wa Mbeya ambapo muitikio wa wananchi ulikuwa mzuri wakafuata na Arusha
baada ya hapa wataenda mkoani Kilimanjaro na kufuatia Mwanza wakimalizia na Dar
es salaam.
Alisema kuwa katika mikoa yote hii wamekuwa wakihimiza
wananchi kupima na kutambua afya zao ,pia wamekuwa wakihimiza wananchi kujiunga
na mfuko huu wa kijamii ambao ndio mfuko pekee wenyewe kutoa mafao saba ambayo yanatosheleza katika
jamii huku akibainisha kuwa zoezi hili ni endelevu kwani litakuwa likifanywa
kila mwaka.
Kwa upande wa mganga mkuu wa mkoa wa Arusha Frida Mokiti
aliipongeza NSSF kwa hatua ambayo wameifikia ya kutoa huduma ya upimaji bure
kwa wananchi kwani alibainisha kuwa wananchi kwani itawasaidia wananchi ambao
hawana uwezo kuliapia matibabu kuweza
kujua afya zao bure
Alitoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Arusha kujitokeza kwa
wingi katika kipindi hichi cha siku mbili kupima afya zao katika uwanja wa
Sherkh Amri Abeid kwani huduma hizi zinatolewa bure na shirika la hifadhi ya jamii
NSSF bila malipo yeyote.