AKUTWA AFARIKI DUNIA KWENYE MAZINGIRA YA KUTATANISHA

MCHIMBAJI mdogo wa madini ya Tanzanite (MwanaApolo) wa mji mdogo wa Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara amekutwa amefariki dunia akiwa pembeni ya barabara kwenye machimbo ya madini hayo.

Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho,Kamanda wa polisi mkoani Manyara,Kamishna msaidizi Liberatus Sabas alimtaja marehemu huyo kuwa ni Jimmy Chawe (25) mkazi wa kitongoji cha Songambele mji mdogo wa Mirerani.

Kamanda Sabas alisema Chawe alikutwa amekufa juzi saa 12:30 asubuhi kwenye barabara iliyopo kwenye machimbo ya madini ya Tanzanite eneo la mpaka wa kitalu D na kitalu C mji mdogo wa Mirerani.

Alisema chanzo cha kifo hicho akija bainika na jeshi la polisi linaendelea na upelelezi ili kubaini chanzo chake .

Alibainisha kuwa mwili wa marehemu umeifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Arusha ya mounti meru najeshi la polisi linaendelea na upelelezi.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post