RAIA WA UJERUMANI AJIUWA KWA KUJIPIGA RISASI KICHWANI

Mtu mmoja raia wa Ujerumani aliyefahamika kwa jina la Klaus Pfattischer(58) mkazi Sangananu amefariki dunia mara baada ya kujipiga risasi

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani hapa Thobiasi Andengenye alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 2:30 usiku katika eneoo la Sangananu  lililopo katika kata ya Usa River tarafa ya Pori wilayani Arumeru  mkoani hapa

Alibainisha kuwa mtu huyo aliyemtaja kwa jina la Klausi Pfattischer ambaye ni raia wa ujerumani alijiuwa  kwa kujipiga risasi kichwani wakati alipokuwa nyumbani kwake.

Alisema kuwa mtu huyo alijiuwa kwa kutumia bastola yake aina ya Heckler yenye namba 78052 

Alisema kuwa tukio hilo lilitokea wakati mke wa marehemu akiwa ametoka nje ya nyumba kwa ajili ya shughuli  nyingine ndipo marhemu alipoingia chooni na kufanya kitendo hicho.

Alibainisha kuwa polisi walifika eneo la tukio na kuchukuwa mwili wa marehemu  na kuupeleka katika hospitali ya kanisa ya seliani kwa  ajili ya uchunguzi zaidi wa madaktari  huku jeshi la polisi likiendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha tukio hilo.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post