CCM ,CHADEMA WAKUTANA NJIA MOJA

Jeshi la polisi mkoani Arusha Juzi lililazika kuwatawanya wananchi ambao ni wafuasi wa chama cha mapinduzi (CCM) pamoja na Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)  mara baada ya vyama vivyo kukutana katika makutano ya barabara wakati vyama hivyo vikiwa vimetoka katika mikutano yao ya hadhara.

Tukio hilo ambalo lilitokea  majira ya saa 12:30 jioni katikaq eneo la Tengeru lililopo katika kata ya Akari wakati wafuasi wa  chama cha mapinduzi wakiwa katika msafara mara baada ya kutoka katika uzinduzi wa kampeni uliofanyika  Usa river   huku wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema wakiwa wametokea katika mkutano wao  wa adhara uliofanyika katika wa chuo cha  Patandi kilichopo katika kata hiyo.

gazeti hili lilizungumza na kamanda wa polisi mkoa Arusha Thobias Andengenye naye alisema kuwa jeshi lake la polisi lililazimika kuzuia fujo ambazo zilisabaishwa na wafuasi wa vyama hivi ambao  walikutana kwa pamoja wakati wakitokea katika sehemu zao za mikukutano ya adhara.

"unajua kilichotokea ni kwamba wafuasi hawa walikuwa wanatokea katika sehemu zao za mikutano nikimaani viwanja vyao vya mikutano na kama unavyojua ccm jana walikuwa wanazindua kampeni zao huko  usa river huku chadema wao wakiwa wameshazindua na walikuwa wametoka katika mkutano wao uliofanyika katika kiwanja hicho cha patandi sasa walivyofika barabarani wakakutana na msafara huu wa ccm ambao ulikuwa unatoka usa kwenye uzinduzi ndo fujo zikaanza hapo''alisema Andengenye

Alibainisha kuwa kwa bahati nzuri polisi walikuwa katika misafari hiyo hivyo walichukuwa hatua ya kuongea na wafuasi hawa na wakawashari wamoja wapo wawaache wenzao wapite kwanza alafu na wengine ndo wapite.

Alisema kuwa pamoja ya kuwa kipindi hicho polisi wanaendelea kuwaomba kuna baadhi ya wanachama walikuwa wakiendelea kutupia na lugha chafu huku wakiwa wanaonyeshana ishara za vyama  lakini hamna hata mmoja ambaye alithurika.

Alisema mara baada ya polisi kumaliza  na kuhakikisha misafara yote imeondoka waliondoka eneo la tukio na hamna mfuasi au mwanachama hata mmoja ambaye anashikiliwa na jeshi la polisi kuhusiana na tukio hilo.

''mara baada ya polisi kuomba na msafar mmoja usimame uache mungine upite hamna mwanachama aliyekamatwa katika swala hilo na waliondoka wote kwa salama salimini'alisema Andengenye

Alitoa wito kwa wananchi kujiepusha na vitendo vya vujo ambazo zitavunja amani na kubainisha kuwa iwapo kuna mtu yeyote yule ambaye ataoneka anachochea uvunjifu wa amani katika kampeni hizi atajwe ili aweze kuchukuliwa  hatua za kisheria mara moja

Na aliwaomba viongozi wa vyama vya siasa mbalimbali ambao vyama vyao vipo katika kampeni hizi kutekeleza ahadi ambazo walizitoa wakti walipokuwa wanaomba ulinzi na waendeshe kampeni za amani ili ziweze kumalizika bila kuleta tatizo lolote.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post