JAMII nchini
imeshauriwa kuvisaidia vikundi vinavyojitolea kufanyakazi ya ulinzi
shirikishi (polisi jamii )kwa kuvipatia msaada wa vitendea kazi ili
kuvipa nguvu na moyo wa kufanya kazi ya kutokomeza uhalifu nchini.
Akizungumza kwa
niaba ya mkuu wa polisi wilaya ya Arusha(OCD ), Zuberi Mwombeji katika
hafla fupi ya kukabidhi Sare kwa ajili ya kikundi cha polisi jamii kilichopo
mtaa wa makaburi ya baniani katika kata ya Unga ltd,vilivyotolewa msaada
na kituo cha Radio cha mambo jambo (MJ FM) cha jijini hapa.
Mkuu wa kituo
cha polisi mjini kati( OCS),Philpo Mzirai alisema hayo muda mfupi baada ya
kupokea sare hizo,na kuongeza kuwa jamii inapaswa kujitoa kwa kila hali kwa
kutambua umuhimu na mchango unaotolewa na vikundi vya polisi jamii
katika suala la kukabiliana na uhalifu ndani ya jamii.
Aidha aliwataka
wananchi waliopo katika maeneo mengine jijini hapa kushiriki vema katika suala
zima la ulinzi shirikishi kwa kuunda vikundi kama hicho,kwani vikundi kama
hivyo maeneo mengi vimeleta manufaa kwa kupunguza uhalifu kwa kiwango kikubwa.
Alitoa ushauri
kwa vikundi hivyo kuepuka kujichukulia sheria mkononi ikiwemo kutumia nguvu
kubwa ,kuwabambikia watu kesi kwa chuki binafsi ,kushiriki vitendo vya
uhalifu na kuwataka kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pindi wanapoona vitendo
vya uhalifu kwenye maeneo yao .
Kwa upande wa
mkurugenzi wa MJ Radio, Kervin Mbogo alisema kuwa amefarijika kwa kikundi hicho
cha polisi jamii,kujitolea kwa kuweka ulinzi shirikishi katika mtaa huo, hivyo
ameona umuhimu wa kukifadhili kwa kutoa msaada huo wenye thamini ya shilingi
700,000 na kuzitaka taasisi,makapuni na watu binafsi kuona umuhimu wa kutoa
mchango wao kwa vikundi kama hivyo.
Aidha alisema
kuwa mchango wake hauta ishia hapo ila anajipanga zaidi katika awamu nyingine
aweze kukabidhi msaada mwingine wa vitendea kazi ikiwemo silaha za moto kwa
ajili ya kukabiliana na ujambazi.
Katika hatua
nyingine jeshi la polisi mkoani hapa,kupitia dawati lake la jinsia na ukatili
limewataka wakazi wa maeneo mbalimbali jijini hapa,kutokaa kimya pindi
wanapoona ama kufanyiwa vitendo vya ukatili wa aina yoyote.
Mkuu wa dawati
hilo,inspekta bi Mary Mmari alivitaka vikundi vya ulinzi shirikishi kusaidia
kufichua vitendo vya ukatili wa kinsia unaofanyika majumbani bila kutolewa
taarifa na badala yake humalizika kimya kimya huku mwathirika akiendelea kuumia
na kuathirika kisaikolojia bila kupatiwa msaada wowote.
Alisema
aliwataja wanawake kuwa ndio wanaongoza kwa vitendo vya ukatili na
kudai kuwa kesi nyingi anazokumbana nazo ofisini kwake zinawalenga wanawake
zaidi kwa kuwanyanyasa watoto wao ama wakambo ,wafanyakazi wa ndani,waume zao
na hata wakwe zao.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia