BREAKING NEWS

Tuesday, March 6, 2012

JESHI LA POLISI MKOANI ARUSHA LAKUBWA NA KASHFA NZITO


Jeshi la polisi nchini limezidi kufanya madudu baada ya kumuuwa kijana moja katika kijiji cha kikatiti  wilaya ya Arumeru mkoani Arusha jimbo ambalo linakabiliwa na vuguvugu kubwa la uchaguzi  kwa kumuusisha na kosa  la kumchoma mwenzake  kisu .

Wananchi wa kijiji alichouwawa kijana huyo waliyomtaja kwa jina la Siriyaeli Peris Kaaya (34) walidai kijana huyo aliuwawa siku ya jumamosi  tarehe 3 march 2012 majira ya saa saba mchana karibu kabisa na kituo cha polisi cha Kikatiti alipokuwa akiishi katika nyumba ya mama yake ambaye ni mwalimu katika wilaya hiyo aliyejitambulusha kwa jina la Elizabeth Peris.

Mashuhuda  wa tukio ilo walidai kuwa kijana huyo alikuwa nyumbani kwake majira ya saa hiyo akiwa amejipumzisha walishangaa askari wawili wa kituo hicho cha kikatiti mmoja wao akiwa amevalia sare za  kipolisi na mwengine akiwa amevaa kiraia ambaye ndiye aliyekuwa ameshika bunduki aina SMG na kuanza kuvunja nyumba  ya mama wa kijana huyo.

Baada ya kuvunja nyumba ya kijana huyo walidai kuwa  walipiga risasi mbili juu na nyingine mbili walimpiga kijana huyo eneo la kiuno na mguu na kumtelekeza  katika nyumba yake jambo ambalo lilimsababishia kijana huyo kuvuja damu nyingi hadi kufariki dunia.
Walidai baada ya kijana Kaaya kufariki dunia polisi walipelekewa taarifa kuwa kijana huyo ndipo polisi walipokwenda kumbeba na kumpeleka katika hosptali ya west Meru iliyoko katia mji mdogo wa Tengeru na kumtelekeza huko bila kutoa taarifa kwa wazazi wake wala ndugui zake.

Mama yake mzazi mwalimu Elizabeth kaaya akielezea tukio ilo kwa waandishi wa habari alisema sike iliyofuata ya tukio alipata habari kutoka kwa jirani yake ambae alisema kuna mama mwenzake ambae alikuwa anatafuta namba ya simu ya mzazi wake na aswa mama yake lakini kwa bahati mbaya hakupatikana mtu mwenye namba ya mama huyo.

Mama huyo alipomuuliza walikuwa wanaitafuta ya nini aliambiwa kuwa walitaka kumweleza kuwa motto wake huyo ameuwawa kwa kupigwa risasi na polisi jana yake katika nyumba yake ya kikatiti kwa kuwa walikuwa na RB yake ya kumchoma mtu na kisu begani.

Alipotaka kujuwa mwanae yuko wapi kwa wakati huo aliambiwa aende katika Hosptali ya Wewst meru lakini hata alipokwenda hakuwewza kumuonyeshwa mweli wa mwanae bali alizungushwa kwa kuambia kuwa aamepelekwa katika hosptali ya mkoa wa Arusha ya Maunt Meru jambo lilimtia shaaka kuwa anaazungushwa ni kweli alishauwawa.

Baada ya kuisi kuwa anazungushwa na mwanae amefariki alienda katika kituo cha polisi cha USA na baada yas kuonana na mku wa kituo pale na kujieleza kuwa ni mzazi wa kijana wake ambae anasikia kuwa amepigwa risasi na polisi na kufariki dunia.

Mkuu huyo wa kituo alithibitisha kuwa ni kweli anataarifa hizo na sababu alizoelezwa na mkuu wa kituo hicho cha kikatiti ni kwamba walikuwa na Rb yake ya kukamatwa lakini polisi walipoenda kukamata alijifungia na wananchi walivunja nyumba kijana huyo alitoka na kisu jambo ambalo lilimfanya askari huyo kujihami kwa kumpiga risasi.

Mama Kaaya alisema hakuridhika na majibu hayo kutokana na taarifa za mashuuda kuwa hakuna wananchi waliyoshiriki kumfukuza kijana huyo bali walishangaa kusikia miliyo ya risasi ambazo za kutishia zilipigwa mbili na za kumpiga zilikuwa mbili na polisi kutokomea bila kumpa huduma hadi alipofariki ndipo walipokuja kumchukuwa.

Mama huyo ilimpasa kuandika barua kwa mkuu wa polisi wilaya ya Arumeru kutaka kupata maelezo ya maandishi kwa jeshi ilo ili kubaini sababu za kuuwawa mwanae na kutelekezwa bila msaada wowote huku hakjua wazi mwanae sio jambazi wala mlevikwa miaka tisa alipomweka mwanae katika nyumba yake aweze kujishuulisha na shughuli za kilimo

 Majirani wa nyumbani kwa kijana huyo ambae ambae anaishi barabarani kabisa na barabara ya moshi wakimzungumzia kijanaa huyo walisema alikuwa kama ana tatizizo la mtindio wa akili kidogo lakini hawajawahi kusikia akipigana wala tabia ya uwizi ingawa alikuwa siku akiwa vizuri anasalimia lakini siku nyingine alikuwa anaweza kukupita .

“huyu kjana hakuwa na matatizo yoyote kabisa ya ugomvi wala kuvuta bangi wala kunywa pombe na kupigana hovyo alikuwa anajishughulisha na kazi zake za kufuga na kulima anaweza kumkuta leo yuko vizuri mkakaa na kuongea nae vizuri na siku nyingine anawezaakapita aongei na mtu akaingia ndani ya nyumba yake akajifungia na kujipumzisha lakini alikuwa hana tatizo na mtu”alikuwa anaongea mama mmoja wa jirani ambae hakutaka kutaja jina lake gazetini.

Akizungumzia tukio ilo kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Lernard Paul ambaye ni mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Arusha, alisema kwa taarifa alizonazo marehemu alimtishia askari ambaye alijulikana kwa jina la koplo Benedkti  alikwenda kumkamata  kwa kutumia kisu jambo ambalo lilimfanya amfatulie risasi ya mguuni na ndipo kijana huyo alipokimbizwa hosptalini huku akitokwa na damu nyingi na kumsababishia mauti.

Alionyesha kisu ambacho marehemu alikamatwa nacho na kukiri kuwa pamoja na kupewa taarifa hizo uchunguzi  kwa ajili ya tukio ilo unaendelea na wanamshikilia Konstebo Benedicti kwa uchunguzi zaidi na kama kuna mabadiliko watayaeleza kwa waandishi wa habari.

Alimyataja kijana aliyechomwa kisu marehemu kuwa Dawson Lyimo ambae alichomwa kisu cha began majira ya saa mbili usiku marchi 2 mwaka huu  na kulazwa hosptali  lakini alishindwa kueleza kuwa amelazwa katika hosptali gani ingawa wananchi wananchi wanadai kuwa yupo nyubani kwake.

Ndugu na jamaa wa marehemu Kaaya walidai kuwa hawatakubali kupokea mwili wa ndugu yao hadi hapo Polisi watakapotoa maelezo ya kutosha ya kifo cha kijana wao aambaye majirani walimweleza kuwa mpole na asiye na matatizo yoyote.



Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates