BREAKING NEWS

Monday, March 12, 2012

CCM YAZINDUA KAMPENI ARUMERU WATU WAFURIKA

Rais mstaafu wa  awamu ya tatu Benjamin Mkapa akiwa anapokelewa na vijana wa Arumeru  wa chama hicho
Mke wa mgombea ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Pamela Sumari akiwa anawasalimia wananchi na kumuombea kura mume wake

Benjamin Mkapa Rais  Mstaafu wa Tanzania hawamu ya tatu  ambaye pia ni mwenyekiti mstaafu wa CCM akiwasili kwenye viwanja vya uzinduzi wakampeni za chama hicho


Mratibu wa kampeni za chama cha mapinduzi jimbo la Arumeru mashariki Mwigullu Nchemba ailiwataka  wananchi wa jimbo hilo kutofanya hasira katika kipindi hichi cha kampeni na baadaye  uchaguzi mdogo wa jimbo hilo kwani wakifanya uchaguzi huu kwa hasira itawapelekea kulipoteza jimbo.


Alisema kuwa wanajua kuwa jimbo la Arumeru mashariki linamatizo makubwa  ambayo yatakiwa kutatuliwa hivyo wachague mtu ambaye ataweza kutatatu matatizo hayo na mtu ambaye anasikilizwa kwa haraka na sio mtu ambaye atachukuwa mda mrefu kusikilizwa.



Aidha aliongeza kuwa ili kupata kiongozi bora kila mwananchi anatakiwa kusikiliza sera za mgombea na kuzipima na kuangalia kama kweli mgombea huyo anayeongea anaweza kutekeleza mambo ambayo ameyasema na iwapo ataona yanafaa ampe kura yake lakini wasikubali kamwe kudanganywa na watu wanaopita  na kupiga kelele za kupanda mwenzake pasipo kusema sera yake na nini atawafanyia wananchi iwapo atachaguliwa.



Pia alisema kuwa katika swala zima la uzushi ambao baadhi ya watu wamekuwa wana lisema kuwa mgombea wa CCM kugombea kwake ni wanaleta uongozi wa kifalme kitu hicho sio cha kwali  kiongozi huyu alitaka kugombea  mara baada ya baba yeke kufariki na sio kabla.



‘’unajua wanasema kuwa eti  mgombea huyu anavyogombea ni anataka kuendeleza uongozi wa kifalme kitu ambacho sio cha kweli na tukiachana na hivyo mbona mbunge ambaye anatoka chadema wa jimbo la Moshi mjini Filimon Ndesamburo yupo bungeni na motto wake pamoja na mkwe wake wote hao ni ndugu lakini sisi atausemi ni uongozi wa kifalme sasa wao huyu mgombea wetu ambaye baba yake mungu kamchukuwa ndo wanasema sasa wananchi nawaambiwa  baba wa kambo akiwa anakuchekea usithanie anakupenda bali anampenda mama yako kwaiyo kuweni makini”alisema Nchemba



Aliwataka wananchi wakiwepo wananchama na wapenzi wa CCM wasikubali kubambikizwa chuki bali watumie vigezo na kumchambua mgombea kwa makini na sio kukurupuka huku akiwasihi wananchama wa chama hicho kuhakikisha ushindi upo wa kishindo na kuwataka wananchi kutafakari kwa makini siku ya kupiga kura na siku hiyo wachague chaguo sahii.



Naye mgombea ubunge wa chama chama mapinduzi Sioi Sumari aliwaomba wananchi hao kuwachagua kwani na kuwahaidi kutekeleza ahadi ambazo mbunge aliyekuwa anaongoza chama hicho aliziaidi  na akuweza kuzitekeleza kwa kipindi hicho.



“changamoto zipo na zinatatulika iwapo tu mtatupa kura zenu na tataweza kuendeleza gurudumu ,uwezo wa kutatua shida ninao nia ninayo cha zaidi ni kura zetu  t undo zitanifanya nipate nafasi hii na niweze kufanya vyote”alisema Sioi



Alitaja baadhi ya vitu ambavyo atavitekeleza iwapo atachaguliwa kuwa ni pamoja na kutatua tatizo la maji ambalo ambalo ndio tatizo kubwa sana kwa wananchi wa jimbo la Arumeru Mashariki haswa sehemu za ngarenanyuki ,kujenga nyumba ya wazee wa mila pamoja na kujenga zahanati hizo ndizo vipo ambavyo atavipa vipaumbele iwapo atachaguliwa .



Pia mgombea huyu alimtambulisha mke wake aliyetambulisha kwa jina la Pamela Solomon Sumari kwa wananchi na wanachama wa chama hicho ambapo alipata fursa ya kuongea ndipo alipowataka wamama  kutoogopa kwenda kupiga kura siku hiyo ya mwisho.




“wakina mama wenzangu napenda kuwasihi sana muende mkapige kura siku ya mwisho msigope kitu chochote kwani hamna mtu wa kuwapiga wala kuwaonea kinachotakiwa ni kuchagua mtu ambaye atawaletea maendeleo na sio mtu wa kuwapotosha  huku akiwashuku wasiogope askari kwani wanalinda amani”alisema Pamela.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates