VURUGU za
Siasa Wilayani Arumeru zimeanza kujitokeza baada ya
vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupiga mawe msafara wa
mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ,waandishi
wa habari na baadhi ya mashabiki wa CCM.
Akizungumza na waandishi wa habari jana wilayani
Arumeru, Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM) ,Martine Shigela alisema UVCCM
inalaani tukio la jana la waandishi kupigwa,mashabiki ,baadhi ya viongozi pamoja
na magari machache kupigwa mawe na mashabiki hao.\
Alisema CCM tangu kwenye uzinduzi
wa kamapeni hizo Machi 12 iliona baadhi ya vurugu zilizofanywa na
Chadema lakini ilikaa kimya ila juzi(jana) vurugu hizo zimejitokeza tena.
Alisema kitendo walichokifanya vijana wa Chadema
ni kitendo kisicho cha kistaarabu na kuwaonya waache mtindo wa kupiga mawe
msafara wa Mgombe wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Sioi Sumari ,mashabiki pamoja na
waandishi wa habari.
Alisema CCM hadi sasa haijampiga mtu hivyo
aliwaomba Polisi kuhakikisha wanasimamia haki na usalama hadi mwisho wa kampeni
za vyama mbalimbali vya siasa na kama Chadema ikiendelea na vurugu zao vijana wa
CCM wataenda msituni kupambana nao.
“Tunaomba polisi kusimamia amani na utulivu na
si kufanya vurugu kwa mashabiki wetu, waandishi wa habari pamoja na kupigamawe
misafaraya viongozi mbalimbali, kama vurugu vitaendelea hizi basi na vijana
wa CCM wataingia msituni”.
Aidha aliwasihi viongozi wa Chadema wafanye
kampeni za kiustaarabu kama walivyoahidi awali na kuwaasa vijana wa chama hicho
kuacha tabia ya kupiga mawe watu wa CCM.
Waandishi walonga
Vijana hao walipiga mawe msafara huo jana majira
ya saa 11:00 na saa 12 jioni eneo la Maji ya Chai ambapo msafara wa CCM ulikuwa
ukirudi mjini kutoka Kata ya Leguruki ambapo mombea Ubunge kwa tiketi ya CCM,
Sioi Sumari alikuwa akimalizia mkutano wake wa mwisho na waandishi wa habari
kuondoka baada ya mkutano huo kuwahisha habari.
Baadhi ya waandishi waliokuwa wakiwahi mjini
kuwahisha habari kwenye vyombo mbalimbali vya habari walisema walipofika eneo la
Maji ya Chai, waliona kundi kubwa la vijana wa Chadema waliokuwa wakisema
wanaondoa mapepo ghafla magari yalisimama na watu kushangaa yawezekana kunaajali
au la.
Mmoja wa waandishi hao, Eliya Mbonea ambaye ni
Mwenyekiti wa Chama cha Waandihi wa habari Mkoani Arusha(APC) alisema walipofika
eneo la maji ya chai waliona vijana wengi ambao walikuwa wakisema wanatoa mapepo
wakati wakiendelea kuangalia kunanini eneo hilo ndipo vijana hao walipiga vioo
vya magari mawe na kujikuta wakiwa katika hali ya taharuki kutokana na fujo
zilizokuwepo eneo hilo.
Alisema wakati wanatafakari nini chakufanya
maana gari limeharibika na wao wapo ndani ya gari dereva alilazimika kutumia
mbinu mbalimbali kupenya katikati ya kundi hilo na kuondoka huku wakiwaacha
wanachama mbalimbali pamoja na viongozi wa chama wakiwa nyuma yao nao
wakitafakari jinsi ya kupita eneo hilo .
|”Ilikuwa ni hali ya hatari baadhi yetu
walijificha chini ya viti kukwepa mawe na wengine wakishindwa kujizuia kutokana
na mshtuko uliotokea wanadai wanatoa mapepo lakini tunawaomba viongozi wa vyama
kuwahamasisha wafuasi wao kufanya kampeni za kistaarabu tunawaomba sana kwani
tunafanya nao kazi kwa karibu hivyo waache vurugu”.
Aliongeza kuwasihi viongozi wa vyama vya
mbalimbali vya siasa kuwasihi wanachama wao kuacha kampeni za vurugu bali
wafanye kampeni za kistaarabu kwani waandishi tunashirikiana na vyama hivyo
vizuri iweje leo hii waanze kuwapiga mawe.
Polisi
Kwaupande wa Polisi walisema kuwa hivi sasa
kunaanza kujitokeza vianshiria vya uvunjifu wa amani kwenye kampeni hizo
kutokana na baadhi ya watu kung’oa bendera vya CCM na Chadema
,kuingiliana kwenye kampeni ,kuchana picha za wagombea,matangazo
ya vyama vingine baada ya saa za kampeni kuisha,wizi wa bendera,kutumia lugha za
kudhalilishana,kuvunja sheria za usalama barabarani kwakuendesha vyombo vya
moto.
Akizungumza Naibu Kamisha wa Polisi
Makao Makuu na Mkuu wa Oparesheni katika Uchaguzi wa
Arumeru, Isaya Mngulu alisema mbali na vitendo hivyo kumekuwa na tabia za vyama
vya siasa nyakati za usiku kuendesha matangazo ya kampeni nyakati za usiku baada
ya muda ulioruhusiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi jambo linaloashiria ukiukwaji
wa sheria,kanuni na taratibu.
Kuhusu matukio ya uhalifu yaliyoripotiwa na
kufanyiwa kazi alisema , hadi sasa matukio matano yamekwisharipotiwa na
kufanyiwa kazi
Matukio hayo ni yanayohusiana na kuchana
bendera/kubandua picha za wagombea.matangazo ya wagombea wa vyama vingine,
matukio mawili yanahusuana na vitendo vya kudhalilishana,tukio moja linahusiana
na kitendo cha kuingilia mkutano wa kampeni wa chama kingine, matukio mawili
yanahusiana na wizi wa bendera pamoja na tukio moja linalohusu ajali ya
barabarani kutokana na mchakato huo wa kampeni.
Alisema matukio manne kati ya matano
yamefikishwa kwenye Kamati ya Maadili iliyopo chini ya Msimamizi wa Uchaguzi
,TrasiasKagenzi na yaliyobakiynafanyiwa uchunguzi wa kina ili yafikishwe kwenye
hatua zinazostahili.
Aliongeza kuwa tathimini ya polisi inaonyesha
kuwa wananchi wa Arumeru Mashariki ni waungwana na hawapendi fujo na alitoa wito
kwa vyama vya siasa ,wanachama,wafurukutwa kuacha vurugu na kuingiliana kwenye
mikutano na waheshimu sheria za usalama barabarani kwani kunaajali
moja imetokea ya pikipiki ambayo imetokana na kutoheshimu sheria za
barabarani.
Alipoulizwa kuhusu polisi
kuziua siasa za matusi zisitokeea kwenye mikutano ya vyama
vya siasa alisema kazi ya polisi ni kuhakikisha usalama unakuwepo eneo la
viwanja vya kampeni na si kudhibiti matusi kwani walengwa wanayohaki ya
kulalamika kuhusu matusi yanayotolewa kwenye Tume ya maadili na si polisi kuzia
matusi hayo kazi yao ni kulinda amani na kuviasa baadhi ya vyama kuacha tabia ya
kupitisha magari yao pale ambapo mkutano wa chama Fulani
unapofanyika.