SIOI ACHUKUWA FOMU KWA AJILI YA KUPATA WATHAMINI

 Sioi akiwa anawasili ofisi ya mkurugenzi wa meru ambaye ndio msimamizi wa uchaguzi
 Akiwa anaingia ofisi ya mkurugenzi huku akisindikizwa na wanachama
 Sioi akiwa anasubiri kuingia kwa mkurugenzi kuchukuwa fomu
 Baadhi ya viongozi wakiwa wanamsindikiza mgombea ubunge kwa mkurugenzi
 mkurugenzi akimkabidhi Sioi fomu



 

 Sioi akiomba kueleweshwa kitu kwenye fomu ambayo alikuwa anakabidhiwa
 Msimamizi wa Jimbo la Uchaguzi,  ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya  Wilaya  ya Meru , Trasias Kagenzi akiwa anamkabidhi fomu za uthamini mgombea ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Sioi Sumary ofisini kwake
 akiwa anazikagua fomu mara baada ya kukabidhiwa
 sioi akifungasha fomu zake mara baada ya kukabidhiwa
 Sioi akiwa na wanachama waliomsindikiza kuchukuwa fomu akiwa anatoka mara baada ya kukabidhiwa
Katibu wa  Chama cha Mapinduzi  Mkoani Arusha, Mary Chatanda wa kwanza kulia akiwa anamnadi mgombea wao kwa wananchama waliomsindikiza kuchukuwa fomu mara baada ya kutoka ndani ya ofisi ya mkurunzi
MGOMBEA Ubunge kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi , Siyoi Sumari jana amechukua fomu kwaajili ya kupata wadhamini wataomdhamini katika  kinyang;anyiro cha kuwania Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki .

Siyoi alichukua fomu hizo leo huku akiwa amesindikizwa na Katibu wa  Chama cha Mapinduzi  Mkoani Arusha, Mary Chatanda , viongozi wa chama hicho pamoja na wanachama mbalimbali ambao baadhi yao walikuwa na pikipiki   huku wakiwa wamefunga bendera za chama hicho.

Akimkabidhi fomu hizo jana  Msimamizi wa Jimbo la Uchaguzi,  ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya  Wilaya  ya Meru , Trasias Kagenzi alisema  fomu hizo zinapaswa kuwa na wathamini wasiopungua 25 hadi 31 na wawe wapigakura ambao waliandikwa kwenye daftari la kupigia kura na wasijitokeze kuthamini wagombea wengine .

Alisema fomu hizo zijazwe kwa ufasaha na n vizuri mgombea akarudisha kwa wakati ili pale kwenye kasoro kuweze kurekebishwa kabla ya kupelekwa kwenye Tume ya Taifa ya uchaguzi. Na kuongeza kuwa mwisho wa kurudisha fomu hizo ni Machi 8 mwaka huu.

Pia mkurugenzi huo alisema mpaka sasa wagombea waliofika kuchukua fomu hio ni sita ambao ni Siyoi (CCM),  Joshua Nassari (CHADEMA) , TLP  Abrahamu Chipaka, DP  Mohamedy  Mohamedy, UPDP  Charles Msuya, SAU  Shabani Kirita.

Alisema kuwa fomu hizo zinapaswa kurudishwa kabla ya machi nane na ifikapo Machi 9 ni siku  ya kuanza  kampeni katika kata 17 za Jimbo hilo , lenye tarafa tatu za Pori , King'ori na Mbuguni.


Alisema kuwa jumla ya wapiga kura walioandikishwa katika daftari la kudumu ni 127,000 na vituo vya kupigia kura vitakuwa 327, japo ana hakika idadi itapungua kwa sababu ya wengine kuhama na baadhi yao kufariki dunia na idadi ya kura zitahesabiwa katika vituo.
Naye Siyoi aliwashukuru wanaCCM waliojitokeza kumsindikiza kuchukua fomu hizo.


Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post