KATIBU Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Dk.Wilbrod Slaa, amewataka wapiga kura wa Arumeru Mashariki, kupuuza kauli za
mbunge wa Jimbo la Mtera (CCM), Livingstone Lusinde za kutaka
watu kumpa kura za huruma Sioi Sumari, ili kumfuta machozi baada ya kufiwa na
baba yake, kwa madai kuwa kura hazitolewi kama fadhila bali zinaamua hatma ya
maisha ya watu.
Dkt Slaa liyasema jana katika kijiji cha Nambala, katika kata ya Kikwe,Wilayani humo, wakati akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chadema, Joshua Nassari.
Alisema ufike wakati watu watambue kura zao ndizo zinazoamua hatma ya maisha yao na hawahitaji kutoa kura zao kwa ajili ya kumwonea huruma mtu kwa sababu ya kufiwa na baba yake, kwa kuwa yeye mwenyewe hajajihurumia kwa kuomboleza msiba huo kwa siku 40 kama ilivyo mila na jadi za Kiafrika.
Akizungumzia kuhusu vipeperushi vinavyosambazwa na jeshi la polisi vya utii wa sheria bila shuruti, alisema inasikitisha kuona IGP na timu yake ikishindwa kuwakamata mafisadi
waliokwapua fedha za wananchi na kuamua kutisha watu kwa kusambaza
vipeperushi vya kutii sheria bila shuruti, ambavyo kimsingi havina
ujumbe wowote ila ni kutisha watu.
Naye Nassari alisema endapo akichaguliwa atawasilisha kero za wananchi
wa Meru kwenye mamlaka husika hususan kwenye Halmashauri na bungeni.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Chadema tawi la Magidrisho, eneo la Usa River, Nuru Maeda (53) ametekwa jana asubuhi na watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CCM na kumbana sehemu ya siri kwa tuhuma za kumkuta na
daftari la wapiga kura.
Akisimulia mkasa huo jana Maeda alisema alifanyiwa unyama huo baada ya
kukutana na Mwenyekiti wa kitongoji cha Magidrisho, aliyemtaja kwa jina la Gerald Kiderio ambaye alimuhoji kwamba alipata wapi daftari la
wapigakura na alipomweleza ni haki kwa vyama vya siasa kuwa nalo kwa ajili ya kuhakiki wapiga kura, alimtaka awasilishe ofisini jambo
alilotekeleza.
Alisema akiwa katika mgahawa wa mke wake jirani na ofisi hiyo, alikuja
kijana mmoja aliyemtaja kwa jina la Ibrahim Idd na kumweleza kwamba
anaitwa na Kiderio na alipofika ofisini kwa Mwenyekiti huyo, ghafla
yalikuja magari mawili mojawapo likiwa na bendera.
Alisema walishuka viongozi wa chama hicho ambao ni Katibu wa CCM
Wilaya ya Moshi aliyemtaja kwa jina moja la Kingazi pamoja na Katibu
wa CCM katika Wilaya moja ya mkoani Manyara ambaye alimtaja kwa jina
moja la Ndekubali ambao walimweka chini ya ulinzi na kumfinya sehemu
za siri ili aeleze alikopata daftari hilo huku wakimnyang’anya.
Alisema wakati vurugu hizo zinaendelea viongozi hao walishauriana
wampeleka ngome ya CCM ambako walimtesa kwa kumpiga na kumjeruhi
lakini walipoona hali imekuwa mbaya ndipo walipompeleka Kituo cha
Polisi cha Usa ambako alipewa fomu ya PF3 kwa ajili ya kutibiwa.
Kamanda wa Operesheni Maalum wa jeshi la polisi katika uchaguzi huu,
Isaya Mngulu, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kwamba jeshi hilo limeanza kuwasaka watuhumiwa.

Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia