TLP YALALAMIKIA RATIBA YA MIKUTANO YA ADHARA

Chama cha TLP kimelalamikia   ratiba iliyoandaliwa na msimamizi wa uchaguzi kwa kudai kuwa ratiba hiyo imepangwa kwa nia ya kuwapa ushindi chama cha mapinduzi.

Akizungumza kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika kwenye kiwanja cha Embaseni  kilichopo katika kata ya maji ya chai mwenyekiti wa mkoa wa chama hicho Leonad makanzo alisema kuwa wanamashaka na ratiba hiyo ya mikutano kwani inaonekana kupangwa kwa nia ya kupendelea chama chama cha mapinduzi.

Alisema kuwa ratiba hiyo imekuwa ikionyesha chama cha mapinduzi kikiwa kinaongoza  kwa kuwa na mikutano mingi zaidi ya vyama vyote na kudai kuwa katika mikutano hiyo chama hicho kimekuwa kikionyesha katika kila siku kitapiga kampeni katika viwanja ambavyo vyama vingine vimepita.

"unakuta kwa siku chama cha mapinduzi kina mikutano mitano alafu chadema ina mikutano miwili na Tlp mmoja alafu kibaya zaidi katika mikutano hiyo unakuta viwanja vilivyopangwa kama sisi tunapiga mkutano asubui basi jioni CCM wanapita na kingine wamechukuwa sehemu nyingi na kama ratiba inavyosema mtu akishachukua kiwanja atakama hata fika chama kingine akiwezi kupiga kampeni sehemu hiyo ivyo ratiba hii inatuumiza sana"alisema Makanzo

Alifafanua kuwa katika ratiba ya mikutano hiyo inaonyesha ccm inaongoza kwa kuwa na mikutano mingi kwani kwa mujibu wa ratiba ina onyesha inamikutano 1961 ,chadema ikionyesha inamikutano 634 na TLP ikionyesha ikiwa inamikutano 26.

"sasa ukiangalia hapo jamani ata kwa macho ya kawaida kwa kupitia mikutano tu CCM si inashinda tu kwa kutumia mikutano pasipo kura jamani si ndo watakusanya watu wote"alisema Makanzo.

Akijibu tuhuma hizi  Trasias Kagenzi alisema kuwa ratiba hiyo haijakosewa kwani wameipanga kutokana na jinzi vyama vimeleta ratiba zao.

Alisema kuwa vyama vyote vilileta ratiba zao na wakazipitia baada yahapo waliwaita viongozi na kuwa pa waka kubali na yeye kama msimazi wa uchaguzi hapangi ratiba bali vyama vyenyewe ndo vinapanga ratiba.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post