TAASISI
ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU)mkoani Arusha
inawashikilia wanachama watatu wa CCM akiwemo aliyekuwa mgombea wa
nafasi ya ubunge katika
jimbo la uchaguzi la Arumeru,mashariki Elirehema Kaaya ambaye ni
katibu
mwenezi wilaya ya Nyamagana , baada ya kuwakuta wakigawa fedha za
rushwa
ili kuwashawishi wajumbe wamchague
mgombea wa nafasi ya uteuzi wa ubunge Siyoi Sumari.
Kwa
mujibu wa mkuu wa Takukuru mkoa wa Arusha Mbengwa Kasomambutu alisema hadi
jana walikuwa wamemtia mbaroni mfanyabiashara maarufu wa madini ya
Tanzanite na diwani wa kata ya Mbughuni Thomas Mollel maarufu kwa jina la
“Askofu” akiwa katika kikao
kilichodaiwa ni mkakati wa kugawa fedha kwa wajumbe wa mkutano walioshiriki
uteuzi wa awali wa nafasi ya ubunge kwa
tiketi ya ccm.
Kasomambutu
alisema askofu Mollel alikabidhiwa fungu la fedha kwa ajili ya kushawishi
kundi la madiwani wa jimbo la Arumeru Mashariki ili wampigie kura Siyoi
Sumari ambapo juzi alikutana na baadhi yao katika kikao ambacho hakikua
rasmi wala halali kwa wakati huu.
Alimtaja mwanachama mwingine wa ccm aliyekamatwa kuwa
ni,Joseph Mollel ambaye ni katibu wa umoja wa vijana wilayani Monduli, wajumbe wa kikao hicho ambaye hakutaka kutajwa jina lake
gazetini alisema kikao hicho hakikumalizika vizuri kutokana na wajumbe hao
kugomea ushawishi huo wakidai kiasi chafedha kinachotolewa ni kiduchu.
“askofu
alifika pale na kudai kuwa yeye ni mjumbe tu na mjumbe hauwawi ila ameombwa
awashawishi wajumbe hao wakubali kufanya ujanja wowote ili kijana huyu
apite halafu mtaona mambo yenu yatakavyonyooka maana Mzee hayupo yupo
Ujerumani jamani”alisema Mjumbe huyo.
Kasumambutu
alifafanua kuwa, mtuhumiwa mwingine aliyekamatwa jana na kuhojiwa ni
aliyekua mgombea wa nafasi ya utezi ndani ya CCM kabla ya uchaguzi huo
kurudiwa leo Elirehema Kaaya(katibu mwenezi CCM Nyamagana) ambae alishika nafasi
ya tatu katika uchaguzi huo.
Alisema
mtuhumiwa huyo ambaye baada ya kuhojiwa amekutwa na tuhuma za kupewa jukumu
la kuwashawishi kwa rushwa wajumbe wote waliompigia kura katika uchaguzi wa
awali wapatao 205 ili wahamishie kura zao kwa mgombea Siyoi ili kumuwezesha
kushinda.
Mmoja
wa wajumbe waliokuwa wakishawishiwa na mtuhumiwa huyo ambae hakutaka jina
lake litajwe gazetini alidai kuwa Elirehema alitumwa na mtoto wa kigogo
mmoja aliyekutana nae Dar es Salaam kuja kushawishi kundi hilo kwaajili ya
kumuwezesha Siyoi kushinda.
Alisema
kwa sasa taasisi yake bado inaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine zaidi
ya watatu waliokimbia katika tukio la jana na kutelekeza pikipiki
walizokuwa wakitumia baada ya kukurupushwa na wenzao kukamatwa, katika
kikoa haramu katika baa iitwayo Levis iliyoko kata ya Maji ya Chai wilayani
Arumeru.
Pamoja
na hili alisema taasisi yake inazishikilia pikipiki mbili zilizokutwa
katika eneo hilo mojawapo ikidaiwa ni ya katibu hamasa wa UVCCM Arumeru John
Nyiti ambae anahisiwa alikuwepo katika kikao hicho na kukimbia.
Kufuatia
kukamatwa kwa watuhumiwa hao Askofu Mollel katika kikao chake na waandishi
wa habari alimtupia lawama mkuu wa mkoa wa Arusha Magessa Mulongo kuwa
ndiye aliyehusika kuwatuma takukuru kuwakamata.
Akijibu
tuhuma hizo Mulongo alisema Takukuru ni taasisi inayojitegemea hivyo hana
mamlaka ya kuwaagiza kufanya kazi na kuwataka wale wote waliokamatwa kwa
tuhuma hizo wajibu tuhuma zao kwa mamlaka hiyo badala ya kuanza kutafuta
mchawi.
Alisema
taasisi hiyo iko kwaajili ya kila mtu bila kujali kuwa yeye ni nani hivyo
mtu hapaswi kuanza kuzua madai yasiyo na msingi kwa kumtuhumu mtu kuwa
anahusika na wao kukamatwa kwakua chama kilionya masuala yote ya rushwa
katika uchaguzi huo.
“mimi
nasema askofu na wenzake wajibu tuhuma zao kama umekutwa ugoni na mke wa
mtu usiseme hapa lazima Fulani anahusika kunitaja bali jibu tuhuma za
kukutwa ugoni na mke wa mtu usitafute mchawi takukuru sisi wote ni wateja
wao”alisema Mulongo.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia